Home Kitaifa FCS NA TCRA CCC WAINGIA MKATABA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WATUMIA HUDUMA...

FCS NA TCRA CCC WAINGIA MKATABA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WATUMIA HUDUMA ZA MAWASILIANO NCHINI.

Na Magrethy Katengu
Dar es salaam

Asasi ya kiraia Foundation for Civil Society (FCS) na Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA CCC) zimewekeana saini ya makubaliano ya miaka mitatu yenye lengo la kuimarisha juhudi za kulinda haki za watumiaji wa huduma mitandao katika sekta ya Mawasiliano nchini Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Agost 6 ,2024 Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bw.Justice Rutenge katika hafla hiyo amesema makubaliano hayo ya umuhimu wa kuwalinda watumiaji dhidi ya mbinu za kibiashara zisizo za haki katika soko kwani hivi karibuni kumeibuka wimbi la utapeli kupitia mitandao ya simu na ya kijamii .

” Ubia huu unalengo la kuhakikisha haki na uwajibikaji katika kutoa Huduma kwa watumiaji na kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi wanaponunua na kutumia bidhaa na huduma za kulinda haki za watumiaji (Consumer Protection)unachangia maendeleo ya masoko na ukuaji wa biashara” amesema Rutenge

Sambamba na hayo ameendelea kufafanua kuwa katika soko la sasa lenye mabadiliko ya haraka,uadilifu katika biashara unategemea kwa kiasi kikubwa kulinda haki za watumiaji dhidi ya mbinu zisizo za haki na udanganyifu katika biashara.

Bw.Rutenge amesema kwamba Wafanyabiashara Wana nafasi muhimu katika kuhakikisha uwazi na usahihi katika shughuli zao,hivyo FCS na TCRA CCC zimeunganisha nguvu katika kubuni na kutekeleza mradi unaolenga kulinda haki za watumiaji wa bidhaa na Huduma za Mawasiliano nchini Tanzania.

Aidha amesisitiza umuhimu wa asasi za kiraia kushiriki katika kuimarisha mifumo ya kulinda na kutetea haki za watumiaji wa uhuduma na bidhaa,nakudai kuwa kwa miaka mingi FCS imekua ikisisitiza maendeleo yaliyojikita katika kuwanufaisha wananchi zaidi.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa TCRA CCC ,Bi.Mary Shao Msuya amesema kwamba Baraza hilo limeanzishwa kwa lengo la Kuhakikisha maslahi ya watumiaji wa huduma za Mawasiliano za TEHAMa,huduma za Utangazaji,Huduma za Posta,na Vifurushi na Vipeto.

Amesema kuwa huduma za Mawasiliano nchini zinaongezeka kutokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia kwa mujibu wa takwimu za TCRA ,kufikia June,2024 kuna kadi za simu milioni 76.6,watumiaji wa internet milioni 39.3,akaunti za pesa mtandao milioni 55.7, ambapo idadi hiyo itaendelea kuongezeka na huduma mpya zitaongezeka kutokana na kukua kwa teknolojia ya kidijitali.

“Ukuaji huu wa teknolojia ni muhimu hasa wakati nchi yetu imejukita kwenye uchumi wa kidigitali ,Mawasiliano yanaweza kufikisha taarifa kwa wakati ,uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo Biashara,uzalishaji ,elimu,afya na upatikanaji wa Huduma jumuishi za kifedha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!