Home Kitaifa FCC YAWATAKA WAKULIMA KUTUMIA PEMBEJEO ZENYE UBORA

FCC YAWATAKA WAKULIMA KUTUMIA PEMBEJEO ZENYE UBORA

Na Monica Sibanda-Dodoma

Mkurugenzi mkuu Tume ya Taifa ya Ushindani William Erio amewataka wakulima kuhakikisha wanatumia Pembejeo zenye ubora ili waweze kulima kwa faida na kupata mazoa yenye ubora.

Hayo ameyasema mara baada ya kutembelea banda la tume hiyo lilipo kwenye maonesho ya Kimataifa ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Amesema wameshiriki kwenye maonesho hayo ili kutoa elimu kwa wakulima,wafugaji na wavuvi ili kutoa elimu ya namna bora ya kumlinda mraji na umuhimu wa matumizi ya pembejeo zenye ubora.

“Tumeshiriki kwenye maonesho haya ili kutoa elimu kwa wadau wote wa kilimo kuepuka matumizi ya bidhaa bandia ikiwemo pembejio za kilimo ili kuhakikisha wanazalisha mazao yenye ubora”,Amesema.

Aidha amesema pia katika maonesho hayo wanawashauri wazalishaji kufungasha bidhaa zao kwa kutumia viwango vilivyothibitishwa na Shirika la viwango la Tanzania (TBS).

Sambamba na haya Erio ametoa wito kwa wananchi na wakulima wote nchi kuhakikisha wanajiandikisha kwenye daftari ya kudumu la wapiga kura ili kushiriki uchaguzi wa serikali na kuchagua viongozi watakao wasaidia kuendeleza kilimo na kuwatafutia masoko ya uhakika.

Amesema kauli mbiu ya maonesho hayo inachochea wakulima kupata viongozi ambao watasaidia kupeleka agenda zao lakini kuwafanikisha kupata masoko Duniani kote.

“Kauli mbiu ya maonesho kwa mwaka huu ‘chagua viongozi bora wa serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo,mifungo na Uvuvi’ imekuja wakati muhafaka tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na serikali kuu hivyo nitoe rai kila mtu alifikisha umri wa kujiandikisha akajiandikishe”,Amesema Erio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!