Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani-Vijijini Aidan Komba (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano, Hamisa Clement mkazi wa Kilosa aliyejishindia kupitia Kampeni ya Magifti Dabo dabo.
Morogoro, 24 Januari 2024: Mshindi wa Kampeni ya Magifti Dabo dabo inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo, Hamisa Clementi mkazi wa Kilosa mkoani Morogo leo amekabidhiwa kitita cha shilingi milioni tano alizojishindia kwenye kampeni hiyo.
Mshindi huyo ameonekana kukabidhiwa mfano wa hundi ya pesa alizojishindia na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani-Vijijini Aidan Komba baada ya kuingiziwa muamala huo kwenye Tigo Pesa yake.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa mfano wa Hundi Hamisa amesema pesa hiyo imekuja wakati muafaka akiwa katika majukumu ya mwezi Januari hivyo pesa hizo zitamsaidia kupunguza ukali wa maisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani Vijijini, Aidan Komba baada ya tukio hilo amewataka watumiaji wote wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Tigo kwa huduma mbalimbali kama kununua bando kwa vocha au Tigo Pesa, kulipa bili, kutumia huduma ya lipa namba, kufanya miamala Tigo kwenda Tigo au mitandao mingine na huduma nyinginezo ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali. Aliendelea kusema;
“Kampeni hii inayoendeshwa nchi nzima bado inaendelea na kuna zawadi mbalimbali bado zinaendelea kutolewa kama vile pesa taslimu shilingi milioni moja, milioni tano, seti ya vifaa vya ndani kutoka kampuni ya madhubuti ya Hisense ikiwemo friji, Tv, microwave na Sound Bar hivyo nawaomba wananchi wote kutumia mtandao wa Tigo ili waweze kuwa washindi.
“Yeyote atakayejishindia vifaa hivyo atamchagua mpendwa wake ambaye naye atapewa bure vifaa kama hivyo alivyojishindia yeye ili kukamilisha maana nzima ya Magifti Dabo dabo”. Alimaliza kusema Aidan.