Home Kitaifa FAMILIA YAMUANGUKIA RAIS SAMIA AWASAIDIE KUREJESHEWA ARDHI WALIYOPORWA

FAMILIA YAMUANGUKIA RAIS SAMIA AWASAIDIE KUREJESHEWA ARDHI WALIYOPORWA

Na Boniface Gideon -TANGA

Familia ya Marehemu Bakari Kidawa wa Jijini Tanga imemumba Rais Samia kuingilia kati mgogoro wao wa shamba kati yao na Uongozi wa Halmashauri ya J iji la Tanga ambao umedumu kwa muda mrefu bila kupata muafaka.

Wakizungumza na Waandishi wa habari jana, watoto hao walieleza kwamba wamelazimika kumuomba Rais Samia aingilia kati baada ya kukosa msaada kutoka kwa mamlaka mbalimbali ambazo zimeshindwa kuwapatia haki yao.

Akizungumza kwaniaba ya familia, Kiongozi wa Familia hiyo Koja Kidawa, alisema kwamba mgogoro huo ulianza mwaka 1,999, wakati ambao marehemu baba yao hajafariki ambapo Kamishna Mkuu wa Ardhi aliziagiza mamlaka za Tanga kuwasikiliza na kuona namna watakavyoweza kuwasaidia kuutatua.

Kwa mujibu wa Koja Kidawa alisema kwamba baadhi ya mashamba ya marehemu baba yako yalichukuliwa na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Mkoa wa Tanga na baadhi ya wafanyakazi wa Serikali bila kuwa na ridhaa ya marehemu baba yao.

Alisema hata hivyo Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Mkoa wa Tanga, lilikanusha kutwaa maeneo yao bali walikiri kugawiwa maeneo hayo na Ofisi ya Mipango Miji baada ya kuomba maeneo hayo ambayo yanapakana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ na eneo la kanga kasera lililojengwa shule ya Binafsi ya Prince and princess.

Aidha alisema baada ya kuona wanapigwa danadana na mamlaka za Serikali mkoani Tanga ambazo, na Ofisi ya Mipango Miji ya Halmashauri ya Jiji la Tanga pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo Dkt Frederick Sagamiko, walilazimika hivyo kwenda Jijini Dodoma kuonana na Kamishna Mkuu wa Ardhi ambaye aliwaandikia barua mamlaka za Tanga kuwahimiza kulitatua suala hilo haraka iwezekanavyo.

Alisema hata hivyo viongozi hao wa Tanga akiwemo Afisa Mipango Miji na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga hawajaonyesha dalili za kutaka kuwasaidia ili wapate haki yao ambayo wanaidai na hivyo kulazimika kufika kwenye vyombo vya habari ili kumuomba Rais Dkt Samia Suluhu kuona namna ya kuwasaidia kutokana na kukosa fedha za kufuatilia suala hilo.

“Katika mgogoro huu tulilazimika kwenda kuonana na viongozi wa mkoa wa Tanga akiwemo Afisa Mipango Miji, Mkurugenzi wa Jiji na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa lakini hawakuonyesha dalili zozote za kutusaidia ndio maana tukaona ni muhimu tukuombe Mhe Rais Dkt Samia Suluhu utusaidia suala hili “Alisema

Kwa upande wake Kidawa Bakari Kidawa alidai kwamba katika eneo lengine la kwao Mipango Miji ililigawa kwa wamiliki wa Shule ya Prince and Princes iliyopo eneo la kange kasera,

“hatuna furaha kabisa na Nchi yetu, kwenye eneo letu la kange,walitupokonya na kuwapatia wamiliki wa Shule ya Prince and princess, wamiliki wanasema wao wamepewa na Halmashauri, lakini Kuna wakati wanasema wanataka watuhamishie eneo la pande”Alisisitiza Kidawa

Kidawa alisema kwamba familia hiyo ina matumaini makubwa na Rais Dkt Samia Suluhu kwamba suala lao litashughulikiwa mapema na kuweza kupata haki yao ya msingi

“Tunamjua Rais Samia Suluhu ni mama mwenye huruma na sisi kama wanawe tunaamini ataingilia kati suala hili ili tuweze kupewa haki yetu “Alisema Kidawa Bakari Kidawa ambaye ni mtoto wa pili wa marehemu.

Hata hivyo jitihada za waandishi wa habari kutaka kupata majibu kuhusiana na sakata hilo kwa mamlaka husika ziligonga mwamba baada ya wahusika akiwemo Ofisa Mipango Miji wa Jiji la Tanga Mussa ambaye alidai hawezi kuzungumzia suala hilo mpaka apate kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Jijini pamoja na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Tanga .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!