Home Kitaifa ETARO SEKONDARI YADHAMIRIA KUWA NA “HIGH SCHOOL” YA SOMO LA KOMPYUTA JIMBO...

ETARO SEKONDARI YADHAMIRIA KUWA NA “HIGH SCHOOL” YA SOMO LA KOMPYUTA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

-MUHONGO KUONGOZA HARAMBEE DISEMBA 23

Na Shomari Binda-Musoma

SHULE ya sekondari Etaro iliyopo kwenye jimbo la Musoma vijijini imekusudia kuwa ” High School” yenye mchepuo wa masomo ya sayansi ya kompyuta kuanzia mwakani.

Hii itakuwa shule ya kwanza kuwa na mchepuo huo kwa mkoa wa Mara na itawasaidia wanafunzi wa shule hiyo kuwa na uelewa zaidi wa masuala ya kompyuta.

Licha ya matarajio hayo ya kompyuta kwa shule hiyo mwakani kwa saaa inazo Maabara za masomo ya sayansi ambazo zimeanza kutumika.

Maabara ya bailojia
Ilishajengwa na tayari inatumiwa huku maabara ya Kjemia serikali imetoa shilingi milioni 30 kwa ujenzi wa maabara hii ambayo itakamilika kabla ya januari 15 mwaka 2024.

Maabara ya Kompyuta
kwa saaa kompyuta 25 zimefungwa kwa msaada ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Northern Illnois, USA.huku shukeani zikitolewa kwa chuo hicho.

Mafunzo ya Kompyuta yameanza kutolewa wiki hii shuleni hapo kwa kutumia Wahadhiri wa DIT ambao ndio wamepewe jukumu la kujenga maabara ya kompyuta.

Mkuu wa shule hiyo Jacob Joseph Chagavalye na walimu wengine wamepongezwa kwa ubunifu wao na udumishaji mzuri wa urafiki wao na Northern Illnois University – mfadhili wa computer lab ya Etaro sekondari.

Maabara ya Fizikia
harambee ya mbunge wa jimbo itachangia ujenzi wa maabara hii ambayo imepangwa ikamilike kabla ya tarehe 1.3. 2024

Etaro Sekondari inajitayarisha (mwakani, Julai 2024) kuwa na Form V yenye mchepuo wa Physics, Mathematics na Computer Science na michepuo mingine ya masomo ya sayansi.

Sekondari ya Etaro ilifunguliwa mwaka 2006 inahudumia vijiji vinne vya Kata ya Etaro. ambavyo ni Busamba, Etaro, Mmahare na Rukuba (Kisiwa).

Etaro Sekondari ina wanafunzi 897. wanafunzi wa Kidato cha nne (Form IV) wanaosoma somo la Fizikia ni 20 kati ya 146 (13.7%), na wale wanaosoma somo la Kemia ni 41 kati ya 146 (28.1%)

Wananchi na wadau wa elimu wanakaribishwa kwenye harambee irakayoongozwa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profeaa Sospeter Muhongo itakayofanyika disemba 23 Kata ya Etaro

Aidha wadau watakaoshindwa kuhudhuria harambee hiyo wameombwa kutuma michango yao kwenye akaunti ya shule hiyo iliyopo benki ya NMB yenye namba 30301200341 jina la akaunti Erato Sekondari

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!