Home Kitaifa ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA YAWAFIKIA VIONGOZI JUMUIYA YA WAZAZI MARA

ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA YAWAFIKIA VIONGOZI JUMUIYA YA WAZAZI MARA

Na Shomari Binda-Musoma

SHIRIKA la Hope For Girls and Women lenye makao makuu yake mjini Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara limetoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wajumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Mara.

Eljmu hiyo imetolewa kwa wajumbe hao kwenye kikao cha kwanza cha baraza hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Mara.

Akitoa elimu hiyo, mkurugenzi wa shirika hilo Robby Samwel amesema wazazi ni walezi ambao wanapaswa kufikishimiwa elimu ya ukatili wa kijinsia

Amesema mkoa wa Mara imepoteza wasomi wengi wskiwemo wasichana kutokana na kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikuwemo ukeketaji.

Robby amesema zipo aina nyingi za ukatili ikiwa ni pamoja na ukatili wa ki ngono, uchumi, kisaikolojia na nyinginezo ambazo kila mmoja anapaswa kupambana nao.

Amesema viongozi wakiwemo wa jumuiya ya wazazi ndio wenye nafasi ya kusemea madhara yanayotokana na ukatili wa kijinsia.

“Naamini mabadiliko yataanzia hapa kwa viongozi wa jumuiya ya wazazi kupitia baraza hili la wazazi mkoa”

Turudi kwenye malezi na tuanze na sisi wenyewe na kikubwa ni kutoa elimu elimu ili kupambana na ukatili wa kijinsia”, amesema Robby.

Wakichangia baada ya kupata elimu kutoka shirika hilo lakini elimu hiyo inspaswa pia kufikishwa kuanzia shule za msingi.

Katibu wa elimu,malezi na mazingira wa jumuiya hiyo Musoma mjini,Asha Muhamed,amesema elimu wsliyoipata wataifikisha kwa jamii ili kupambana na ukatili wa kijinsia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!