Home Kitaifa ELIMU BIMA YA AFYA KWA WOTE YAANZA KUTOLEWA

ELIMU BIMA YA AFYA KWA WOTE YAANZA KUTOLEWA

Wizara ya afya nchini Tanzania imeanza kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa bima ya afya kuanzia ngazi ya zahanati hadi ngazi ya hospitali ya taifa Muhimbili. Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa mipango wizara ya afya Bw. Edward Mbanga wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kupitia utaratibu huo wa bima ya afya kwa wote, bima za afya zinaenda kuboreshwa.

Kulikua na tatizo ambalo kwa kweli wananchi walishatuambia kama serikali na tumeliona kwamba kuna baadhi ya wananchi walikua wanajiunga na bima ya afya hasa CHF wanaenda kwenye vituo hawapati huduma au wanakosa dawa au wanapata mapokezi ambayo hawakuyatarajia “

Nipende kutumia fursa hii kwamba kupitia utaratibu huu wa bima ya afya kwa wote serikali imejipanga dawa zinapatikana za kutosha wahudumu wanatoa huduma za afya na tutawawekea misingi ambayo watahakikisha wanatoa huduma bora za afya”

Hata hivyo bima inayoyolewa na mfuko wa taifa wa bima ya afya ina mafungumafungu ambapo kuna vifurushi ambavyo havina baadhi ya huduma na vifurushi ambavyo vina huduma

Unaweza kujiunga na vifurushi viitwavyo najali,au wekeza au timiza kuna baadhi ya vifurushi havina baadhi ya huduma cha kwanza wekeza hakina baadhi ya huduma,timiza ndio kina huduma nyingi zote”


“Tunachoenda kufanya kama sheria hii watapitisha wabunge hakutakuwa na vikundi vya mafao,ukishajiunga kila kitu kilicho kwenye kitita cha msingi unakipata”

Aidha kwa kuzingatia mahesabu huduma nazo zinagharama ili hospitali ziendelee kutoa huduma lazima mwananchi achangie na serikali ichangie kwa kiwango ambacho kitatoa huduma hizo.

Kwa upande wake kamishna wa bima Tanzania Bw. Baghayo Sakware amesema kuwa wataongeza aina nyingine ya watoa huduma kwa maana yakusimamia hospitali ambazo zitatoa huduma za bima

Sisi tutakua tunasimamia na kukagua mara kwa mara kama mteja wetu wa bima amepata kitita kilichoahidiwa katika mfumo wa bima ya afya ya umma au kampuni ya bima binafsi”

Ametoa wito kwa wananchi kuamini serikali na sheria itakayokua mkombozi kwa watanzania ili waweze kupata huduma ya afya kwa kupitia bima ya afya wakati ambao mwananchi hana hela mfukoni.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!