Home Kitaifa EFM WAJIBU MASWALI AMBAYO YANAULIZWA MTANDAONI KUHUSU DINA MARRIOS NA OSCAR OSCAR

EFM WAJIBU MASWALI AMBAYO YANAULIZWA MTANDAONI KUHUSU DINA MARRIOS NA OSCAR OSCAR

Meneja wa vipindi EFM Dickson Ponela ametambulisha kipindi kipya cha JIONI YA LEO kitakacho kutanisha watangazaji wa vipindi mbalimbali kwenye kituo hiko akiwa na imani kitaleta mapinduzi makubwa kwenye vipindi vya jioni.

Utambulisho wa kipindi hiko kiliambatana na kutambulisha Watangazaji hao kwa majina akiwepo Dina Marrios, Oscar Oscar, Roman Shirima, Mpoki na Veronica Frank.

Pia Mkurugenzi wa Uendeshaji Denis Sebo alisema Dina Marrios alijiunga EFM miaka saba iliyopita na alijijenga na kujulikana kama mwanamke wa shoka na aliweza kuunganisha timu ya uhondo ameweza kuanzisha Boss mama, Raha za uswahilini, Kitchen part gala.

“Oscar Oscar alijiunga nasi miaka saba iliyopita kitaaluma ni mwalimu, ametengeneza mahusiano mzuri zaidi ya kazi akaweza kutumia vizuri mitandao yake ya kijamii”amesema Sebo.

Pamoja na hayo Dina Marrios amesema alianza kipindi cha UHONDO kilianza kwa kulenga wanawake nashukuru EFM kwa kumpa ushirikiano mpaka kufikia kuhamia kipindi cha JIONI YA LEO .

Vilevile Oscar Oscar amesema amefundisha Sekondari kwa muda wa miaka mitano ,akafanya kazi taasisi ya elimu ya juu akafanya kazi chuo kikuu kwa muda wa mwaka mmoja akahamia EFM kwa kushikwa mkono na Maulid Kitenge .

“EFM kwangu kama maisha imenikuza Maulid Kitenge anamchango mkubwa sana katika maisha yangu amenitoa kwenye ualimu hadi kuwa mwandishi wa habari mwaka huu ninahitimu Shahada yangu ya Uandishi wa habari “amesema Oscar Oscar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!