Home Kitaifa DR KIJAJI AWAHASA FCC NA WAFANYABIASHARA KATIKA KUHITIMISHA SIKU YA USHINDANI DUNIANI

DR KIJAJI AWAHASA FCC NA WAFANYABIASHARA KATIKA KUHITIMISHA SIKU YA USHINDANI DUNIANI

Katika kuhitimisha siku ya ushindani Duniani iliyoenda sambamba na kaulimbiu isemayo ‘Njama baina ya washindani na madhara yake‘, Waziri wa Viwanda na Biashara, Daktari Ashatu Kijaji ametoa agizo kwa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) na vyombo vingine vinavyosimamia masuala ya biashara kutekeleza majukumu yao kwa kuongeza nguvu ya utoaji elimu kwa wafanyabiashara na kuwaelekeza zaidi kuhusu masuala ambayo wanapaswa kutenda ili kuepusha uvunjaji wa sheria.

Tuendelee kutoa elimu kwa wazalishaji wenyewe lakini pia kwa walaji ili tuendelee kuelewana juu ya athari kubwa za kufifisha ushindani ndani ya Taifa letu” Alisema Kijaji

Aliongeza kuwa “Mbinu ambazo si halali zina athari hasi, huwa wakati mwingine tunafikiria ni athari hasi kwa watumiaji lakini muda mwingine hata kwako wewe mfanyabiashara au mzalishaji zile mbinu ambazo si halali zinaweza kukunufaisha kwa muda mfupi lakini kwa muda mrefu zinaweza zinakuaribia soko, Lazima Sheria ziwepo ili zisimamie vitendo hivi visiwepo kwani vinatuathiri sisi wenyewe,” aliongeza Kijaji.

Daktari Kijaji aliwataka wawakilishi na wadau wafahamu kuwa madhumuni ya serikali ya awamu ya 6 katika kusimamia uchumi wa soko, si kukataza biashara bali ni kutaka ifanyike kwa kuzingatia sheria na misingi ya ushindani, pia washindani wanatakiwa kushindana kwa uhuru na amani na Si kula njama za kukwepa kushindana sokoni ili kutimiza malengo yaliyowekwa na sheria ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyo bora.

Kijaji alisema sheria ya ushindani ina umuhimu mkubwa sana katika kujenga uchumi wa Taifa hivyo wafanyabiashara wanapofanya biashara zao kwa kufuata misingi ya sheria wataweza kuongeza ufanisi katika uzalisha na usambazaji wa bidhaa na huduma lakini pia wataweza kukuza ubunifu ikiwa ni wa kuboresha matumizi ya raslimali kwa kuzingatia vipaumbele.

Aidha alisema Kukosekana kwa ushindani ndani ya soko hudumaza ukuaji wa uchumi kwani wawekezaji wengi huvutiwa kuja kuwekeza nchini hivyo ni vyema kushirikiana ili fursa zilizopo nje ziweze kuletwa katika soko la ndani.

Lazima tushirikiane, fursa zilizopo nje ziletwe ndani na tuzalishe tukiangalia soko kubwa tulilokuwa nalo nje, tujipange tunaendaje kushindana kwenye soko la Afrika, AGOA nchini marekani,” alisema.

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), William Erio alisema Msingi wa kuadhimisha siku ya ushindani Duniani ni kutekeleza adhimio la baraza kuu la umoja wa mataifa katika kikao chake cha mwezi April 1980 ambacho kilipitisha taratibu na kanuni za kudhibiti vitendo vinavyofifisha ushindani katika biashara ulimwengu.

Katika kutekeleza kaulimbiu ya mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha maadhimisho haya tumetekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo kufanya mikutano na waandishi wa Habari lakini pia semina mbalimbali kuhusu uelewa wa masuala ya ushindani, tumetoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya FCC na maadhimisho ya siku hiu katika Kanda 4 nchini,” alisema Erio.

Alisema kupitia mikutano hiyo walipokea mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wadau na ambapo mapendekezo hayo watayafanyia kazi kwa mujibu wa taratibu za kiserikali.

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI), Bw. Leodgar Tenga alisema wafanyabiashara hawana budi kufanya biashara zao kwa kufuata sheria za ushindani kwani kwa kufanya hivyo mlaji na mtumiaji ataendelea kufaidia kwa kupata bidhaa na huduma bora katika bei inayo aksi uhalisia.

Tenga alisema kwa mfanyabiashara itamsaidia kupata ufanisi katika uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma lakini pia kukuza ubunifu vitu vitakavyopelekea kukua kwa uchumi wa nchi.

Pia Tenga alisema uwepo wa sheria ya ushindani imeleta faidha nyingi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa wawekezaji ndani na nje ya nchi yetu kupitia muunganiko wa Makampuni hivyo kuongeza pato la Taifa na ajira kwa wananchi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!