NA MWANDISHI WETU
Katika kufikia lengo la maisha Bora Kwa kila mtanzania anapata huduma ya lazima Kama afya , Elimu na Ustawi wa Jamii katika Halmasha ya Wilaya Kisarawe.
Akizungumza wakati wa ukaguzi na Ufunguaji wa miradi leo 03.01.2023 Kisarawe Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dr Selemani Jafo amesema ameridhishwa na Maendeleo yanafofanywa katika Maeneo yake katika Kata ya Chole,Masaki, Maneromango,na Marumbo,
“Binafsi Maendeleo ya Jamii yangu yananipa Faraja Sana Nikilinganisha na Tulivyokua hapo awali”
“Maendeleo haya yote Ni jitihada za Pekee za Rais wangu kwa watu wangu wa kisarawe katika kuwaletea Maendeleo hatuna budi kumpongeza na kumuombea Dua pamoja na viongozi wakuu wote katika Kuijenga Tanzania alisisitiza Mhe Dr Jafo“
Ukaguzi huu wa miradi ya Maendeleo kisarawe husaidia kuona Jamii ni jinsi gani Serikali ya Dr Rais Samia Na Chama cha Mapinduzi Ccm kinavyowajali wananchi wa Kisarawe kwa vitendo.
Aidha Ukaguzi huu wa miradi ya Maendeleo Ni Mwendelezo wa utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi Ccm kwa vitendo Kisarawe
KAZI IENDELEE