Na Magrethy katengu
Kituo Cha Uwekezaji TIC kimesema katika kipindi Cha mwaka 2021Juni hadi Julai 2022 kimefanikiwa kusajili miradi 274 ikilinganishwa na miradi 234 katika kipindi hicho cha mwaka 2020/2021 na kufikia ongezeko la asilimia 14.6.
Akizungumza leo Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kituo Cha Uwekezaji TIC John Mnali amesema miradi hiyo iliyosajiliwa katika kipindi hiko inatarajiwa kuzalisha ajira 43,925 ikilinganishwa na ajira 36,470 zilizoripotiwa kipindi cha mwaka 2020/2021.
“Miradi tuliosajili ipo katika sekta ya Viwanda,Usafirishaji,Kilimo,Ujenzi/Majengo ya biashara,miundombinu ya kiuchumi,Taasisi za fedha ,raslimali watu,usafirishaji,Utalii na huduma nyingine“amesema Mnali
Hata hivyo amesema takribani miradi 6 inatarajiwa kuwekezwa yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.10 itazalisha ajira 28,7 na kuokoa fedha za kigeni zaidi ya dola za Marekani bilioni moja ambazo zingetumika kuingiza bidhaa hizo kutoka nje ya nchi.
Mnali alibainisha miradi hiyo kwa kuitaja Itracom limitedi Uzalishahi mbolea,Bagamoyo sugar limited kilimo cha Uzalishahi sukari,Kagera sugar limited,Mtibwa sugar,Knauf Gypsum limited Uzalishahi wa Gypsum powder na Gypsum board,Taifa gas uchakataji na usindikaji wa ges.
Hata hivyo TIC imeendekea kuhamasisha Uwekezaji wa ndani na nje Kwa kushirikiana na Ofisi za kibalozi na Ofisi ya Waziri Mkuu na kupokea wawekezaji huku miundombinu ikiboresha ikiwemo Barabara,bandari,viwanja vya ndege,reli na umeme hivyo hufanya kupitia makongamano ya Uwekezaji.