Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kuzungumza na Uongozi wa Umoja wa Watu wenye Ulemavu waendesha Bajaji kutoka Mkoa wa Dar es Salaam (UWAWABADA).
Viongozi hao waliomtembelea katika ofisi yake jijini Dodoma kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujadiliana kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazowakabili katika sekta hiyo.
Aidha, Katika kikao hicho viongozi hao na wajumbe wa UWAWABADA wametoa pongezi zao kwa Waziri pamoja na Ofisi yake kwa namna wanavyo shughulikia masuala mbalimbali yanayowakabili Watu wenye Ulemavu ili kuimarisha ustawi wa kundi hilo.