Home Kimataifa DKT. TULIA AHIMIZA MAPAMBANO DHIDI YA MABADILIKO YA TABIANCHI NA KULINDA AMANI...

DKT. TULIA AHIMIZA MAPAMBANO DHIDI YA MABADILIKO YA TABIANCHI NA KULINDA AMANI YA DUNIA

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wanachama wa Umoja huo kudumisha misingi ya IPU ikiwemo kuendeleza amani na usalama, kulinda misingi ya demokrasia, kuchagiza Mabunge jumuishi, kulinda usawa wa kijinsia na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Tulia ameyasema hayo wakati akifunga rasmi Mkutano Mkuu wa 148 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Geneva (CICG), nchini Uswisi leo tarehe 27 Machi, 2024.

Aidha, amesisitiza Viongozi wa Mabunge wanachama kuona umuhimu wa kutoa taarifa za utekelezaji ndani ya Mabunge yao juu ya maazimio ya Mikutano Mikuu yanayopitishwa ili kuleta matokeo chanya kwa jamii wanayoiwakilisha.

Vilevile amesema kuwa, IPU ni sehemu pekee ambayo Mabunge yanakutana kwa pamoja kupitisha maazimio yanayoihusu dunia na hivyo ni muhimu kwa Maspika wa Mabunge wanachama kuhudhuria Mikutano ya Umoja huo.

Mkutano wa 148 umehitimishwa rasmi leo huku ukiwa umehudhuriwa na takribani misafara ya Mabunge zaidi ya 145.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!