Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa ajili ya kutekeleza azimio la Mkutano Mkuu kuhusu uteuzi wa wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Kikao hicho, kilichofanyika leo tarehe 19 Januari 2025 katika ukumbi wa NEC maarufu kama White House, kimepitisha jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea wa nafasi ya urais kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.