Home Kitaifa DKT. PINDI CHANA AONYA WANAOVUNJA SHERIA ZA UHIFADHI

DKT. PINDI CHANA AONYA WANAOVUNJA SHERIA ZA UHIFADHI

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema wapo watu wachache wanaovunja sheria za uhifadhi kwa makusudi na wengine kwa kutokujua sheria, hasa wafugaji wanaoingiza mifugo kwenye Hifadhi za Taifa na mapori ya akiba yaliyo kwenye Kanda ya Kusini.
Waziri Chana amewataka wahifadhi kusimamia vyema sheria za uhifadhi ili kukabiliana na baadhi ya watu wachache wanaofanya uharibifu katika maeneo ya Hifadhi nchini na kusisitiza kuwa sheria zilizopo zisiposimamiwa kikamilifu madhara yatakuwa makubwa sio tu kupoteza sifa za hifadhi hizo bali kupunguza idadi ya watalii.

Awali akiwasilisha taarifa za utekeleza wa majukumu na hali ya uhifadhi wa Pori la Akiba la Mpanga Kipengere, Mhifadhi Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Alfred Kipondamali, amesema moja ya mafanikio yaliyopatikana ni kusaidia jamii inayozungula pori hilo kwa kuchangia vifaa vya ujenzi wa shule na kituo cha afya katika Kijiji cha Mpangampya

Kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi ya Kitulo inayosimamiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Theodera Aloyce, amewashauri madiwani wa mkoa wa Njombe kushirikiana na taasisi hiyo hasa katika kuchangamkia fursa zitokanazo na utalii Kanda ya Kusini katika kutoa huduma kwa watalii kutokana na matokeo chanya ya Filamu ya Royal Tour.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!