Home Kitaifa DKT.MWINYI ATAKA MABALOZI KUTANGAZA FURSA ZILIZOPO NCHINI.

DKT.MWINYI ATAKA MABALOZI KUTANGAZA FURSA ZILIZOPO NCHINI.

Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dkt Hussein Mwinyi amewataka Mabalozi walioteuliwa hivi karibu kuiwakilisha Tanzania katika Nchi za Zimbabwe, Zambia na Uholanzi, kufanya juhudi za kuitangaza nchi pamoja na kuangalia fursa za kiuchumi.

Dkt.Mwinyi ametoa wito huo Ikulu Zanzibar alipokutana na Mabalozi hao akiwepo Balozi.Simon Siro (Zimbabwe) Lt.Jen.Mathew Mkingule (Zambia) na Balozi. Caroline Chipeta anaeiwakilisha Tanzania nchini Uholanzi waliofika Ikulu kuaga.

Amesema kuna umuhimu mkubwa kwa Mabalozi hao kuitangaza vyema Tanzania katika Nchi hizo kwa kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo pamoja na kuangalia fursa mbalimbali za Kiuchumi.

Alisema katika kuendeleza diplomasia ya uchumi Serikali imeweka kipaumbele sekta za uchumi wa Buluu kwa lengo la kukuza uchumi wake, hivyo alisisitiza umuhimu wa kuzifanyia kazi fursa zilizomo katika sekta hizo.

Dkt.Mwinyi alimtaka Balozi wa Tanzania Nchini Uholanzi Mhe. Caroline Chipeta kuweka nguvu ili kuongeza idadi ya watalii wa Nchi hiyo wanaozuru nchini.

Aidha Dkt.Mwinyi aliwata Mabalozi hao kuchangamkia fursa za masoko ya mazao ya Karafuu na Viuogo kwa kuwaunganisha wafanyabiashara wa nchi hiyo pamoja na wa Zanzibar.

Katika hatua nyingine Dkt.Mwinyi aliwataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika Nchi za Zimbabwe na Zambia kuendeleza Uhusiano na Ushirikiano wa kihistoria uliopo kwa kuangalia fursa za kibiashara zilizopo pamoja na kuangalia suala la Ulinzi na Usalama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!