Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli Ikulu Zanzibar aliyefika kujitambulisha baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan tarehe: 28 Disemba 2023.
Rais Dkt.Mwinyi amesema Zanzibar sekta kuu ya uchumi ni utalii ni fursa kwa Uganda kufanya biashara na uwekezaji pamoja na fursa nyingine zilizomo katika uchumi wa buluu .
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amemtaka Balozi Simuli kudumisha ushirikiano na kubadilishana taarifa za ulinzi na usalama eneo la mpakani kati ya Tanzania na Uganda.
Naye Balozi Simuli amempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kazi nzuri anayoifanya kuibadilisha Zanzibar kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.