Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema anatarajia kufanya mageuzi makubwa ndani ya chama atakaposhika hatamu ya uongozi nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar
Ameyasema hayo leo baada ya kushiriki kwenye uchaguzi wa nafasi mbalimbali za Uongozi wa chama katika ngazi ya Wilaya ya Amani uliofanyika kwenye Ukumbi wa Amani Mkoa uliopo Mkoa wa Mjini Magharibi*
Dk.Mwinyi amesema zimebaki hatua mbili za uchaguzi ndani ya chama ikiwemo Mkoa na Taifa ili kufanya mabadiliko ya uongozi ambapo baada ya kukamilika hatua hizo na kuwa Makamu Mwenyekiti amebainisha kuyafanya mageuzi