Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ameendelea na ziara yake ya kupokea na kutatua changamoto papohapo jimboni humo, ambapo siku ya jana amefanya ziara kata za Doromoni, Kidaru na Kisiriri.
Akiwa katika maeneo hayo Dkt Nchemba amesikiliza changamoto, maoni na kero mbalimbali za wananchi hao na kuzipatia utatuzi papohapo. Maelfu ya wananchi wa Jimbo hilo wameendelea kumiminika katika ziara hiyo inayoendelea katika viunga mbalimbali vya wilaya ya Iramba.
Dkt Nchemba ameambatana wa Viongozi wenzake mbalimbali wa wilayani humo wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda, Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi Iramba na Madiwani wa Halmashauri hiyo.