Home Kitaifa DKT. MWIGULU AKIPONGEZA CHUO CHA MIPANGO KWA KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI.

DKT. MWIGULU AKIPONGEZA CHUO CHA MIPANGO KWA KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Dkt. Remidius Ruhinduka, alisema Chuo cha Mipango kikiwa ni Chuo pekee hapa nchini chenye jukumu la kuandaa watalaamu wa masuala ya mipango ya maendeleo kitaendelea kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi wa hali ya juu.

Dkt. Ruhinduka aliongeza kuwa Chuo kitaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata Sheria, Taratibu, Kanuni na Miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali mara kwa mara na kuendelea kutoa wahitimu mahiri na wenye kutumia weledi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katika mahafali ya 37 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) wahitimu 6,362 ambapo wanaume ni 2,783 na wanawake ni 3,579 wametunikiwa Astashahada, Stashahada, Shahada ya kwanza, Stashahada ya uzamili na Shahada ya uzamili.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!