Home Kimataifa DKT. MPANGO: WATANZANIA TUMIENI FURSA HII KUJIFUNZA NA KUPATA UZOEFU.

DKT. MPANGO: WATANZANIA TUMIENI FURSA HII KUJIFUNZA NA KUPATA UZOEFU.

Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Nchi za Umoja wa Ulaya linalofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 24 Februari, 2023 limefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akifungua Kongamano hilo, Makamu wa Rais amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi wananchama wa Umoja wa Ulaya kuja kuwekeza nchini kwenye maeneo yanayoendana na mahitaji ili kuiwezesha Tanzania kutimiza malengo ya Dira ya Taifa ya 2025 na kukuza kutoka uchumi wa kati wa chini hadi uchumi wa kati wa katikati.

Akianinisha maeneo mbalimbali ambayo wawekezaji hao wanaweza kuwekeza, Dkt. Mpango amesema Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji ambazo wanaweza kuwekeza ikiwemo kilimo, viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo, viwanda vya dawa na vifaa tiba, ujenzi, sayansi, teknolojia, maendeleo ya viwanda katika kizazi cha nne ( 4) ( 4th Industrial Evolution).

Aidha amesema Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa kuendelea kurekebisha sheria, kuboresha mifumo ya ulipaji kodi ikiwemo sera za ulipaji kodi kwa nchi kumi, kuimarisha kituo cha uwekezaji Tanzania ( TIC) na Mamlaka na Mamlaka ya kukuza Uwekezaji  Zanzibar (ZIPA), Kuimarisha upatikanaji wa umeme, Uendelezaji wa Bandari ya Dar es salaam, Tanga na Mtwara, Bandari kavu ya kwala , ujenzi wa barabara na reli, na uanzishaji wa Sheria ya Uwekezaji ya 2022 ikifuta ile ya 1997

Dkt. Mpango amesema Serikali imefanya jitihada mbalimbali za kuifungua nchi kwa uchumi wa Dunia kwa lengo la kuifanya tanzania kuwa kitivo cha biashara na uwekezaji na kupanua biashara Kujifunza, kubadilishana uzoefu kufahamiana na kutafusa fursa na kuingia makubaliana kibiashara

Ufunguzi wa kongamano hilo ulihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi kutoka Tanzania wakiwemo Mawaziri wa sekta za uzalishaji akiwemo waziri wa nchi Ofisi ya Rais Uchumi, Kazi na Uwekezaji wa Zanzibar Mhe. Mudrick Soragha ,Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbalawa, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu , Manaibu Makatibu Wakuu, Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Umoja wa Ulaya akiwemo Mhe. Balozi Jestas Abouk Nyaman, Wakuu wa Taasisi za umma na sekta binafsi pamoja na wajumbe wa kamati ya Viwanda, Biashara Kilimo na Uvuvi.

Aidha viongozi wa Serikali na Taasisi kutoka na umoja wa Ulaya wamehudhuria akiwemo Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini tanzania Mhe. Manfredo Fanti, Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na vivutio vya uchumi wa Ufaransa Mhe. Olivier Becht; Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Ulaya huduma za nje Bi Helena Konig na Makamu wa Rais wa Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya Mhe.Thomas Östros,

Katika hotuba yake Waziri wa Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na vivutio vya uchumi wa
Ufaransa Mhe.Olivier Becht ameainisha nia ya nchi yake kuimarisha uwekezaji Tanzania na Afrika Mashariki na jinsi Serikali yake imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania hususan katika sekta za kimkakati

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya (EIB) Mhe. Thomas Ostros amesema Benki hiyo imerudi nchini baada ya UVICO- 19 na iko tayari kufanya uwekezaji mkubwa wenye thamani ya EUR milioni 540 kwa kuwawezesha wawekezaji na wafanyabiashara nchini wakiwemo wananwake , maji, utalii na na kampuni zinazojihusisha wna uchumi wa blue, hii itafanyika kupitia ushirikiano wa kifedha kati ya EIB na CRDB, NMB, na KCB pamoja na makubaliano yaliyofanyika leo kati ya makampuni ya Umoja wa Ulaya na Tanzania makampuni ya Tanzania itakayowawezesha kuwekeza na kupanua biashara zao hususani katika utalii, uvuvi.

Katika kongamano hilo hati za makubaliano nne (4) zimetiwa saini ambapo Hati ya Makubaliano ya Huduma ya Usafiri wa Anga uliotiwa saini na Waziri wa ujenzi na uchukuzi Mhe. Prof Mbalawa na Waziri wa mambo ya nje, biashara na vivutio vya uchumi wa Ufaransa Mhe. Olivier Becht ambapo makubaliano hayo ytawezesha kuongeza idadi ya safari za ndege kati ta tanzania na ufaransa ikiwemo safari moja kwa moja kutoka dar es salaam kwenda ufarasa ifikapo mwezi june 2023 kisiwa cha mayotte ambapo makampuni ya ndege ya tanzania yataruhusiwa kusafiri moja kwa moja hadi kisiwa hichokwanza Tanzania and French direct Zanzibar to France

Hati nyingine ya makubaliano iliyotiwa saini ni kati ya bandari ya Antwerp-Bruges International na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania ambao utaongeza usimamizi wa bandari na kuimarisha miundombinu ya bandari ikiwemo bandari kavu na bandari za maziwa na kuiongezea uwezo bandari hiyo ili kuongeza ufanisi wa bandari ya Tanzania

Hati ya makubalioano ya tatu ilihusu ujenzi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa Kakono Hydro Power utakaojengwa Mkoani Kagera uliofadhiliwa na Benki ya Maendelo Afrika chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya, hati ya nne ni kati ya Knauf Gypsum Tanzania Limited Kisemvule, Mkuranga inayopanga kupanua uzalishaji wa gypsum 6

Kongamano hilo limejumuisha zaidi ya washiriki 800 kutoka nchi za Umoja wa Ulaya na Tanzania linalenga kuwaunganisha washiriki hao katika kongamano linalolenga kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na wawekezaji wa Tanzania watapata fursa ya kujadiliana na wafanyabiashara wenzao wa Umoja wa ulaya katika maeneo ya kilimo, Nishati Uzalishaji, Ujenzi, usafirishaji na Mawasiliano Mikutano ya majadiliano kati ya serikali na wafanyabiashara
.
MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!