Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amezindua mradi wa maji wa Sibwesa wilayani Tanganyika Mkoani Katavi.
Mradi huu ni sehemu ya ufanikishaji wa Kampeni ya Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO 19 katika sekta ya maji na umegharimu milioni 173.2.
Mhe Mpango ameipongeza Wizara ya maji kwa kusimamia utekelezaji wa mradi huo na kusisitiza waendelee kujipanga zaidi ili chanzo cha uhakika cha maji ya Ziwa Tanganyika kitumike kwa ajili ya huduma ya maji katika mkoa wa Katavi.
Awali akiongea katika hafla hiyo Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema mradi huo unapanuliwa zaidi ambapo shilingi bilioni 1.8 zimetengwa kwa kazi hiyo na mkandarasi ameshapatikana. Amesema lengo la Wizara ni kuhakikisha wananchi wa Sibwesa, na taasisi zote zilizoko katika eneo la mradi wanapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza.