Home Kitaifa DKT.MPANGO ATAKA MIRADI YA MAJI ISIMAMIWE, BEI YA NISHATI YA GESI IPITIWE

DKT.MPANGO ATAKA MIRADI YA MAJI ISIMAMIWE, BEI YA NISHATI YA GESI IPITIWE

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Wizara ya Maji kufuatilia matumizi ya fedha za miradi ya maji na kuchukua hatua kwa wote ambao wanashindwa kutumia fedha kama ilivyopangwa.

Dkt. Mpango amesema hayo jijini Mbeya wakati wa Mkutano mkuu wa nane wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde uliofanyika katika hoteli ya Eden Highland, jijini Mbeya.

Mkutano huo umehusisha uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti rafiki kwa vyanzo vya maji katika chanzo cha maji cha Nzovwe, na itafanyika kitaifa.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesisitiza miradi ya maji isimamiwe vizuri kwa sababu wananchi wanahitaji maji, hivyo ili kunusuru vyanzo vya maji ni muhimu kubadili tabia za watu kwani wanachangia katika uharibifu wa vyanzo hivyo.

Pamoja na hilo, ameongeza kuwa ipo haja ya kuangalia bei za nishati, ikiwamo gesi ili wananchi waweze kumudu bei yake badala ya kutegemea nishati ya mkaa ambao unachochea ukataji wa miti na kuharibu mazingira.

Dkt. Mpango amesisitiza pia ufugaji wa kisasa uwe kipaumbele na wakulima wapimiwe mashamba ya mifugo na sio kuzunguka nchi nzima, kwani mifugo ikizurura inaharibu mazingira.

Pamoja na hayo, ametaka wananchi wote waliojenga katika milima ambayo ni vyanzo vya maji wapatiwe maeneo mengine na wahame katika maeneo hayo.

Amesisitiza suala la utunzaji wa vyanzo vya maji na kuviendeleza kuwa ni jukumu la wananchi wote

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!