Home Kitaifa DKT. MPANGO AITAKA WIZARA YA UWEKEZAJI KUONDOA VIKWAZO VYA KIBIASHARA

DKT. MPANGO AITAKA WIZARA YA UWEKEZAJI KUONDOA VIKWAZO VYA KIBIASHARA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameielekeza Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kusimamia uondoaji wa vikwazo vinavyokwamisha biashara ya Tanzania katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) ili kurahisisha ufanyaji biashara baina ya nchi hizo.

Dkt. Mpango ameyasema hayo wakati akifunga rasmi Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya kibiashara yaliyoanza tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022 jijini Dar es salaam ambapo alitembelea baadhi ya mabanda ya Taasisi na Wafanyabiashara ili kujionea bidhaa na Teknolojia zinazotumika katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Makamu wa Rais pia amezielekeza Taasisi za Masoko za Zanzibar na Bara kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushieikiano wa Afrika Mashariki kushughulikia changamoto za masoko na vifungashio vyenye ubora vya bidhaa za Tanzania, upatikanaji wa malighafi za baadhi ya bidhaa ikiwemo bidhaa za mafuta ya kula.

Vilevile, amezitaka taasisi za utafiti kufanya kazi za ziada ya kutafiti mbegu bora za mafuta ya kula zenye kutoa mafuta mengi zaidi.

Dkt. Mpango pia ameyataka Makampuni ya simu kushirikiana na Taasisi kuwekeza katika teknolojia za kidijitali zaidi.

Aidha, ameitaka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara kufanya tathimini ya maonesho ya Sabasaba ili kuboresha maonesho yajayo na ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kukaa na sekta ya fedha kuangalia namna watu wanavyoweza kupata mtaji kwa ajili ya biashara na uwekezaji.

Dkt. Mpango amewasisitiza Wafanyabiashara Kuzingatia kanuni za ushindani kwa kuheshimu mikataba na kuwataka waongeze uzalishaji kwenye bidhaa zenye mahitaji makubwa nchini kama sukari, mafuta ya kula na vifaa vya ujenzi ili nchi iweze kujitosheleza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!