Home Afya DKT LUSASI: IFIKAPO 2025 MAAMBUKIZI YAPUNGUE NA KUFIKIA ASILIMIA 3.5

DKT LUSASI: IFIKAPO 2025 MAAMBUKIZI YAPUNGUE NA KUFIKIA ASILIMIA 3.5

Na. Magrethy Katengu

Imeelezwa kuwa Tanzania kwa Sasa Hali ya Ugonjwa wa Malaria ni asilimia 94 ambapo maambukizi lakini kwa mwaka 2017 ilikuwa ni asilimia 7.5 ya maambukizi hivyo Serikali lengo ni kufika asilimia 3.5 mwaka 2025 ili kupunguza vifo vitokanavyo Malaria.

Akizungumza kwenye Semina ya siku ya waandishi wa habari iliyofanyika Jijini Dar es Salaam kuelekea katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani tarehe 25 April,2023 Jijini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kaimu meneja mpango wa Taifa wa kudhibiti malaria kutoka wizara ya Afya Dkt. Abdallah Lusasi amesema hali ya maambukizi, vifo, pamoja na wagonjwa wanao lazwa kutokana na ugonjwa wa malaria imeshuka na kuonesha mafanikio makubwa katika kuelekea mpango wa kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.

Tunapoelekea katika maadhimisho ya siku ya maleria Duniani, Serikali ya Tanzania imejipanga kuja na mipango ya afua za kukabiliana na ugonjwa huo ikiwemo kuanza kutoa Dawa kinga kwa watoto kuanzia miaka 0 ili kufikia malengo ya maambukizi kwa asilimia 0″ amesema Dkt Lusasi

Sanjari na hayo pia kuna mikakati zaidi ya kupambana na Malaria ikiwemo upatikanaji wa Dawa na vyandarua, kupitia kitengo cha kampeni ya mapambano dhidi ya Marelia na kitengo cha utafutaji fedha na usimamizi wa miradi ya Malaria.

Nae Mratibu wa Udhibiti wa Malaria Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Ford Chisongela, amesema kaya zisizokuwa na kipato juu ndiyo hukabiliwa na ugonjwa WA malaria ambapo katika mkoa huo licha ya kuwa ni miongoni mwa mikoa inayofanya vyema katika kudhibiti malaria bado wana hitaji kuja na afua za kukabiliana na ugonjwa huo ikiwemo kugawa vyandarua kwa watu wasiojiweza ili kuhimiza matumizi ya vyandarua.

Tuko asilimia 0.7 sawa na Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Dodoma, Iringa na Njombe, kwa hiyo tumepiga hatua sana lakini moja ya mambo ambayo yametuwezesha kufika huko ni matumizi ya vyandarua.

“Dar es Salaam ilianza kunyunyizia viuwadudu kwenye mazalia ya mbu mwaka 1996. Mikoa mingine wameanza miaka mitatu iliyopita hii imesaidia kupunguza kiwango cha maleria pamoja na matibabu ambayo tunawapa wananchi wetu.

Ukiangalia Kiwilaya Ilala inaongoza kuwa na Maleria, Kimkoa tukiwa na asilimia 0.7 wenzetu Ilala wana asilimia 1.7, kwa hiyo wao ndio wanaongoza wakifatiwa na Kinondoni na Ubungo ambazo Takwimu zao zinafanana, kisha Tameke na Kigamboni wao wana maambukizi kidogo,”amemaliza Chisongela.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Rashid Mfaume akizungumza wakati akifunga Semina hiyo ya Waandishi wa Habari amesema Mkoa huo upo tayari kwa maadhimisho ya kitaifa ya malaria na ameainisha mipango katika kuahakikisha inapunguza maambukizi kwa kata ya Msongora Ilala, na tungi Kigamboni, ambazo bado zina maambukizi ya juu licha ya kuwa miongoni mwa mikoa tisa iliyo chini kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

Aidha maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani mwaka huu inatarajiwa kufanyika April 25 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam yakiwa na Kaulimbiu isemayo ‘WAKATI WA KUTOKOMEZA MALERIA NI SASA, BADILIKA, WEKEZA, TEKELEZA’ Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

ZIRO MALARIA INAWEZEKANA WAKATI NI SASA”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!