Home Biashara DKT. KIJAJI: WATANZANIA TUMIENI FURSA KUUZA BIDHAA UINGEREZA

DKT. KIJAJI: WATANZANIA TUMIENI FURSA KUUZA BIDHAA UINGEREZA

Serikali imewashauri Watanzania kutumia fursa ya Mpango wa Biashara wa Nchi Zinazoendelea kwa kuhakikisha wanauza bidhaa kwa uadilifu na ubora katika soko la Uingereza ili kukuza uchumi na pato la Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) Machi 28, 2024 alipokuwa akifungua Warsha ya Wafanyabiashara kuhusu fursa ya kuuza bidhaa katika soko la Uingereza na Nchi zinazoendelea (UK- DCTS).iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Aidha, .Dkt. Kijaji amesema Mpango huo umeanza kutumika 2023 ambapo Serikali ya Uingereza iko tayari kupokea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa Tanzania, zikiwemo zenye kulipiwa ushuru na zisizolipiwa

Amebainisha kuwa kwa mwaka 2022 mauzo ya Tanzania kwenda Uingereza yalifikia sh. bil 44 ikilinganishwa na manunuzi ya sh. trilioni 3.08 ya bidhaa kutoka Uingereza.

Aidha, ametolea mfano taarifa ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kuanzia mwaka 1997-2024 jumla ya miradi 980 ya Kampuni ya Uingereza yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 5655.38 zilizotoa ajira za wastani wa watu 126,322 katika sekta mbalimbali ziliwekezwa nchini

Tuweze kutumia mpango huo na kuchochea mapato pamoja na fedha za kigeni, lakini pia kupitia mpango huo Taifa litakuwa na manufaa mbalimbali ambayo ni kupungua kwa masharti ya kupeleka bidhaa na kwa wenye viwanda ni muhimu kuwa na malighafi zitakazochochea ushindani wa bidhaa za Tanzania,” Amesema Dkt. Kijaji

Ameongeza pia manufaa ya mpango huo ni kupungua kwa gharama za kufanya biashara kurahisisha upatikanaji wa taarifa za masoko kwa Tanzania na hata kushirikiana na kampuni za Uingereza kuwekeza na kuzalisha bidhaa bora Tanzania

Naye Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Cancar amesema chini ya mpango huo Tanzania ndio yenye bidhaa zinazotakiwa na Uingereza na kutakuwa na ongezeko kubwa la biashara baina ya nchi hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!