Home Biashara DKT. KIJAJI APONGEZA JUHUDI KUBWA ZINAZOFANYWA NA RAIS SAMIA

DKT. KIJAJI APONGEZA JUHUDI KUBWA ZINAZOFANYWA NA RAIS SAMIA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) leo tarehe 09 Septemba, 2023 ametembelea kiwanda cha kutengeneza vioo cha Sapphire Float Glass kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani kwa lengo la kuona maendeleo ya hatua za ujenzi wa kiwanda hicho cha vioo.

Dkt. Kijaji amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha mazingira ya biashara yaliyopelekea kujengwa kwa kiwanda hiki cha kutengeneza vioo ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100.

Vilevile Dkt. Kijaji ametoa pongezi kwa uongozi wa kiwanda hicho kwa kufanikiwa kukamilisha ujenzi wa kiwanda hicho kikubwa ndani ya miezi kumi na moja. Kiwanda hiki kinatarajia kuajiri wafanyakazi wa kudumu 1,650 na wafanyakazi wa muda 6,000.

Kiwanda cha Sapphire Float Glass kinatarajia kuanza uzalishaji mwezi huu wa Septemba, 2023 na bidhaa za kiwanda hicho zinatarajiwa kuuzwa ndani na nje ya nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!