Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amewahimiza na kuwahamasisha wafanyabiashara wa Saudi Arabia kuongeza kasi ya kununua bidhaa kutoka Tanzania pamoja na kuja kuwekeza nchini
Waziri kijaji ameyasema hayo Aprili 29, 2024 alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mauzo Nje wa Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Al Thukair alipokuwa akishiriki Mjadala kuhusu mageuzi ya nishati duniani wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaloendelea Jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Kwa upande wake Mkurugenzi huyo ameahidi kuongoza ujumbe wa wafanyabiasha na wawekezaji wakubwa kuja nchini Tanzania kwa lengo la kujionea fursa hizo.