Home Kitaifa DKT. KIJAJI AKERWA NA TAASISI ZA SERIKALI ZENYE MAMLAKA YA UDHIBITI KUENDELEA...

DKT. KIJAJI AKERWA NA TAASISI ZA SERIKALI ZENYE MAMLAKA YA UDHIBITI KUENDELEA KUFUNGIA BIASHARA NA VIWANDA NCHINI

Na Scolastica Msewa, Dar es Salaam

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji ameonyesha kukerwa kuendelea kufungwa kwa biashara na viwanda kupitia Taasisi za serikali zenye mamlaka ya udhibiti viwanda na biashara kwasababu ya changamoto mbalimbali za Wafanyabiashara kwani shughuli za biashara na viwanda zinaendelea kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa wakati sheria ilikwisha zuia hatua hiyo kuchukuliwa kwenye viwanda na biashara nchini.

Amesema hayo wakati akifungua mkutano ulioambatana na Maonyesho ya biashara ya Wakala wa Usajili wa biashara na Leseni BRELA na Wadau wake uliofanyika Mlimani city jijini Dar es salaam ikiwa ni mkutano wa kwanzakufanyika.

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 kupitia sheria ya fedha ya mwaka huu jumla ya sheria na kanuni 17 zimefanyiwa marekebisho, sheria ya fedha hiyo mwaka 2023 imeweza kupunguiza na kufuta jumla ya tozo, ada na faini 97 lengo ni lile lile ya serikali yetu ya awamu ya sita kuhakikisha mazingira ya ufanyaji biashara yanakuwa bora kabisa.

“Kwa upande mwingine katika sheria ya mwaka huu 2023/24 kupitia sheria ya fedha tukimsikia Waziri mwenye dhamana ya fedha alisema vizuri kabisa ilikuwa ni kuzuia kufungwa kwa biashara na viwanda taasisi zetu za udhibiti”

“Hapa naomba ni sisitize na kutoa rai kwa mamlaka zote za serikali za udhibiti ziendelee kuhusu biashara zifanye kazi hata kama kuna jambo hatukubaliani kati yetu lakini wakati tunashughulikia jambo lile hakuna sababu ya kusitisha shughuli za biashara kwani kusitisha biashara ni kusimamisha uchumi wa nchi” amesema Dkt. Kijaji.

“Ni muhimu sana wakati tunapoelekea kuhitimisha mkakati wa dira ya maendeleo wa mwaka 2025 msisitishe shughuli yoyote ya kiuchumi kwa jambo lolote lile kwani mazungumzo ndio msingi wa sisi kuwa na uchumi imara tunapoongea biashara au kiwanda kinaendelea kufanya kazi hilo ni la msingi mno”

Alisema zipo baadhi ya taasisi ambazo pamoja na katazo hilo wanaendelea na kufungia viwanda na biashara.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ameaamua kuwabeba wafanyabiashara wetu, ameamua kuwalea wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambao wapo ndani ya Tanzania hivyo tusifanye mdhaa na maamuzi haya ya muhimu ya Dkt. Samia Suluhu Hassani” “Unajambo lako muite muhusika kaanae shughuli za kiuchumi ziendelee kutengeneza ajira za vijana wetu na kuendelea kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa letu”

“Niwaombe wafanyabiashara na wenye viwanda mliopo hapa na watakao nisikia baadae nimekabidhiwa jukumu la kuratibu sekta hii simu yangu ipo wazi masaa 24 taasisi yoyote ya serikali ya udhibiti inayokuja kukufungia biashara au kiwanda hata kama ni saa nane usiku nipigie simu tushughulike ili uendelee na kazi yako”

Mwenyekiti wa Bodi ya ya ushauri ya BRELA Prof. Neema Mori amesema Lengo kuu la Mkutano wa BRELA na wadau wake ni Kuimarisha mawasiliano baina ya BRELA na Wadau wake ili kujenga uelewa wa huduma zinazotolewa na BRELA pamoja na kupata mrejesho wa ubora wa huduma hizo.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA GODFREY NYAISA mkutano huo mkubwa wa BRELA na wadau wake utakuwa ukifanyika kila mwaka na ushirikishwaji utazidi kuwa mpana zaidi. Nyaisa amesema katika mkutano huo kutakuwa na mijadala itakayohusisha shughuli za BRELA ikiwa ni pamoja na Usajili wa Makampuni, Majina ya Biashara, Miliki Ubunifu na Utoaji Leseni.

++++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!