Home Kitaifa DKT INTERNATIONAL TANZANIA WAADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KWA KUTOA ELIMU YA...

DKT INTERNATIONAL TANZANIA WAADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KWA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA KINGA N AFYA  YA UZAZI 

Mkurugenzi wa Kampuni ya DKT International Tanzania ambao ni watengenzaji wa Kinga (condom) pamoja na vidonge vya kupanga uzazi kushoto akiwa Mkuu wa idara ya Mauzo wa Kampuni hiyo Deograthius Kithama pamoja na wafanyakazi wa Kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kusheherekea siku ya ukimwi duniani

WADAU wa Afya ya uzazi pamoja na watoaji elimu ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi  wawakumbusha watanzania kuendelea kutumia kinga ili kupunguza kasi ya Maambukizi ya mgonjwa ya zinaa.

Akizungumza na Michuzi Mkurugenzi Mkuu wa DKT International Tanzania  Kevin Hudson amesema katika kuunga mkono jitihada za kupambana na maambukizi ya ukimwi Kampuni hiyo yenye dhamana ya kutengeneza kinga hizo(condoms) kwa kipindi cha mwaka 2021 iliweza kuchangia takribani kinga milioni 900 katika kuhakikisha inapiga vita maambukizi hayo.

Kama Moja ya wadau wakubwa duniani katika uzazi wa mpango, DKT International Tanzania inaunga mkono jitihada za siku ya Ukimwi duniani Dkt imechangia kinga (condom) takribani Millioni 900 kwa mwaka 2021 pekee.”

Hudson ameeleza namna mipango yao  kwa Kampuni dhidi ya vita ya maambukizi hayo ni kutilia Mkazo wa kuboresha Maisha ya watu kwa “kwa kujikinga kwa raha” (making safety fun).

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Mauzo Kampuni ya DKT International Tanzania ambao ni watengenzaji wa vidonge vya Afya ya uzazi pamoja bidhaa Kinga (condoms),Deograthius Kithama amesema Kampuni hiyo imekuwa miongoni mwa wadau wakubwa wakijikita kutoa elimu kwa jamii kupiga vita maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Hata hivyo ameeleza kuwa DKT International Tanzania imekuwa ikitumia watu maarufu kama mabalozi katika kuleta ushawishi na uelewa juu ya matumizi ya kinga (condoms) pamoja na Afya ya uzazi ili na kuhamasisha michezo kwa vijana (cycle for hiv) ili kuwafikia vijana kwa urahisi kwani vijana wamekuwa miongoni mwa rika ambalo linaongoza kwa maambukizi hayo.

Tumekuwa tukitumia majukwaa mbalimbali pamoja na matukio kama “world kissing day” ambayo tulitumia moja ya bidhaa zetu aina ya “Kiss condom ‘ katika kueleza umuhimu wa kujikinga na ukimwi,hata hivyo tulitumia watu maarufu kama mabalozi katika ushawishi na uhamasishaji wa kutumia kinga akiwemo  Msanii Idris Sultan, Calisah ,Maggie vampire na kuhakikisha tunashiriki michezo  ya kuendesha bicycle visiwani zanzibar. “

Vilele tumekuwa tukijikita pia kutoa elimu ya Afya uzazi kwa namna gani wapenzi watapanga idadi ya watoto watakaoweza kuwahudumia huku wakiwapa nafasi ya ukuaji sahihi usioleta madhara ikiwemo kukosa lishe na ukuaji imara .

…Mwisho..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!