Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo anashiriki Sherehe ya kuwekwa Wakfu na Kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo jipya Katoliki la Mafinga, Ndg. Vincent Cosmas Mwagala.
Sherehe zinafanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Kiaskofu jimboni Mafinga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Jimbo hilo jipya la Mafinga limezaliwa kutoka Jimbo la Iringa.