Home Kitaifa DKT. AYUBU RIOBA: VYOMBO VYA HABARI VYA AFRIKA SHIRIKIANENI NA KUBADILISHANA MAUDHUI

DKT. AYUBU RIOBA: VYOMBO VYA HABARI VYA AFRIKA SHIRIKIANENI NA KUBADILISHANA MAUDHUI

Na Magrethy Katengu– Dar es salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkkt. Ayubu Rioba Chacha amevishauri vyombo vya habari vya Afrika kushirikiana na kubadilishana maudhui badala ya kuchukua kutoka taasisi za Magharibi taarifa ambazo zimekuwa na mitazamo ya nje na mara nyinyi zinabagaza Afrika.

Ushauri huo aliutoa jana Julai 12, 2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kusaini makubaliano yaliyofanikiwa kati ya TBC na sauti ya Nigeria (VON) ambapo amesema Nchi za Afrika zimekuwa zikibagazwa sana hasa na vyombo vya Magharibi kwani ikiangaliwa kwa makini ni mtazamo uleule uliokuwepo enzi na enzi umeendelezwa sasa ifike wakati Uzalendo uanzishwe kupitia mashirikiano ya kubadilishana maudhui.

“Afrika ikishirikiana kiuchumini itakuwa na mafanikio makubwa sana hivyo naamini tutakaposhirikiana wenyewe kwa wenyewe tutakuwa tunaandaa maudhui na tunarusha taarifa chanya na kuweka katika mitandao ya kijamii maudhui ambayo yatakuwa yanaakisi mitazamo yetu ya kiafrika” amesema Rioba

Hata hivyo Rioba amebainisha kuwa TBC imefanya kielelezo na vyombo vingine havina budi kuiga kwani makubaliano hayo yatasaidia kukuza lugha adhimu ya kiswahili na kupata watangazaji wa lugha hiyo, kuzalisha wataalamu wa kufundisha na kutoa mafunzo ya kiswahili.

“Shirika la utangazaji Tanzania limekuwa na uhusiano mzuri na mashirika na taasisi mbalimbali za habari na utangazaji katika bara la Afrika kupitia makubaliano haya yataleta tija kubwa ya kukuza ajenda ya Afrika kutokana na umuhimu utakaoonekana kwa kuelezea masuala yanayohusu mazuri ya nchi za Afrika” amesema Dkt. Rioba

Hata hivyo, Rioba amesema ili kuhakikisha wanakuwa na ushirikiano wa kudumu kati ya Tanzania na Nigeria darasa la lugha ya kiswahil limeanzishwa nchini Nigeria ili wawekezaji wa nchi hiyo waweze kutumia lugha hiyo wanapotembelea Afrika Mashariki na kumekuwa na mazungumzo ya kushirikiana mafunzo ya lugha ya kiswahili na chuo cha Port Harcourt pia chuo kikuu cha Ghana kutoa Shahada ya lugha ya Kiswahili.

Pia amesema makubaliano waliyoingia leo yana historia ndefu toka enzi za Rediao Tanzania Dar es salaam (RTD) kupitia idhaa ya kingereza (external services) ilikua na ushirikiano wa karibu na shirika la utangazaji Nigeria (Nigeria broadcasting corporation-NBC) kupitia idhaa ya matangazo ya nje ambazo zilishinikiza shughuli za ukombozi barani Afrika .

“Baada ya bara zima kupata uhuru ushirikiano huu ulififia kutokana na mabadiliko yaliyotokea katika mfumo wa kisiasa na kiuchumi duniani kudhoofisha umoja wa nchi za Afrika husika kuanza utegemezi katika nyanja mbalimbali kutoka mataifa ya nje hususani Ulaya Marekani” amesema Ndace

Aidha ili kuhakikisha Tanzania mazuri yake yanasemwa huko Duniani TBC inatarajia kuanzisha chaneli ya mtandaoni itakayotangaza habari kwa lugha ya kingereza kuelezea mazuri yanayotekelezwa na bara la Afrika.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa VON Bw. Jibrin Ndace amesema wanashukuru kwa fursa hiyo ambayo itasaidia kukuza ajenda ya Afrika kutokana na umuhimu ulioonekana kwa waafrika wenyewe kuelezea masuala yanayowahusu kwa mitazamo yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!