Home Kitaifa DIWANI MWANDARA AZUNGUMZIA MIAKA 2 YA MAFANIKIO KATA YA BWERI

DIWANI MWANDARA AZUNGUMZIA MIAKA 2 YA MAFANIKIO KATA YA BWERI

Na Shomari Binda-Musoma

DIWANI wa Kata ya Bweri, Dickson Mwandara, amesema yapo mafanikio makubwa ya miradi ya maendeleo iliyofanyika Kata ya Bweri kwenye kipindi cha miaka 2.

Mafanikio yaliyotajwa kwenye mafanikio hayo ni kwenye sekta ya elimu, miundombinu, maji, afya na miradi mingine.

Katika mkutano wake wa hadhara na wananchi wa mtaa wa Songe diwani huyo amesema katika sekta ya elimu yspo mabadiliko makubwa ikiwemo ujenzi wa madarasa kwenye shule za msingi na sekondari.

Amesema madarasa hayo yaliyojengwa yamepelekea watoto wsliokuwa wakikaa chini kusomea sehemu salama na kupata elimu yao

Diwani huyo amesema zipo shule mpya 2 ambazo zinajengwa eneo la Bweri Bukoba ambazo zinakwenda kuimalisha suala la elimu

Akizungumzia suala la miundombinu,Mwandara amesema katika Kata ya Bweri barabara nyingi zimefunguliwa na kupitika na kuwanufaisha wananchi.

Amesema serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,amekuwa akitoa fedha nyingi zikiwemo za miradi ya miundombinu na kuishukuru serikali

Kwenye afya amesema dawa zimekuwa zikipatikana kituo cha afya Bweri na uboreshaji mkubwa umefanyika kwenye eneo hilo Kata ya Bweri.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wameshukuru mkutano huo wa diwani kuhusu miradi ya maendeleo na kusisitiza hali ya ulinzi na usalama pia liangaliwe

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!