Home Michezo DIWANI MTAMBALIKE AZINDUA OFISI ZA KLABU YA BUNJU MBWENI 

DIWANI MTAMBALIKE AZINDUA OFISI ZA KLABU YA BUNJU MBWENI 

VIJANA watakiwa kuwa sehemu ya kuhamasisha desturi ya kufanya Mazoezi na kutumia vizuri mitandao ya Kijamii katika kuhamasisha jamii imashiriki Mazoezi mbalimbali ya viungo.

Diwani wa Kata ya Mbweni Single Mtambalike amesema kupitia Serikali yake atahakikisha Michezo inapewa nafasi kubwa kutokana na Michezo imekuwa sehemu ya kusaidia jamii, kuhakikisha Afya za watu zina imarika na Kurudisha tabasam kwa wagonjwa mahospitalini kutokana na michango inayotolewa kwa baadhi ya taasisi na makampuni mbalimbali. 

Mtambalike ameeleza kwa namna klabu hiyo ya Bunju Mbweni ilivyojitengeneza kuanzia gropu la watu wachache mtandaoni hadi kufikia kuwa Klabu kubwa yenye Wanachama zaidi ya 15.

“Klabu yenu imekuwa kadri siku zinavyokwenda na leo mmekamilisha zoezi la kuwa na Ofisi ambapo pale mtakapohitajika au watu wanataka kujiunga na klabu hii watakuja moja kwa moja Ofisi zenu hapa Mbweni bunju vile niwapongeze kwa hatua kubwa mliyo onyesha ya kuhakikisha mnapiga hatua nakuona ipo haja ya wanachama kuongeza ili muwe na nguvu kubwa katika Mashirikiano ndani ya klabu”.

Aidha Mtambalike ametolea ufafanuzi alichoombwa na Rais wa Klabu hiyo uhitaji wa eneo la wazi kwa ajili ya Mazoezi  (Open space) ili kuwaleta wana mazoezi karibu badala ya kutoa nje mji kutafuta Maeneo ya kufanya Mazoezi ambapo kwa upande wa wazee na watoto limekuwa likiwaletea changamoto. 

Maeneo ya wazi (Open space) yapo mengi  hivyo sasa nawapa kazi ya kutafuta eneo ambalo mtaona linafaa warudi kwangu kunipa mrejesho wa hilo eneo ili tufanye mchakato wa kuwamilikisha eneo hilo kuwa rasmi kwa Mazoezi kwa wakazi wa Bunju  Mbweni kwa faida ya watu wote hata sisi viongozi tutakuwa sehemu ya kufanyaMazoezi eneo hilo litakalopatikana.”

Kwa Upande wake Rais wa Klabu hiyo Ibrahim Sultan ameainisha mipango ya klabu hiyo ni Kushirikiana na jamii kwa matukio mbalimbali ambayo yatahakikisha michezo inapewa nafasi kubwa ili kuweka miili vizuri na kuepukana na maradhi mbalimbali.

Hata hivyo amewaasa wenye magroup ya mitandaoni na makundi ya vijana kuhakikisha umoja wao unakuwa msaada na tija kwenye jamii zao.

“Klabu yetu ilianza ikiwa kwenye mtandao wa whatsapp lakini tukaona ipo haja tujitanua na tuwe na klabu ambayo itatumika kuwaleta vijana karibu katika mazoezi na tayari tumeshashiriki mashindano mbalimbali nje ya mikoa hivyo utaona kwa jinsi gani Klabu ya Bunju Mbweni tumeamua kuwa rasmi na kuhakikisha michezo inapewa nafasi na tupo tayari kuwapokea wanachama wenzetu wapya.”

Hata hivyo amesema kilio chao kikubwa ni kuona Klabu hiyo inatengeneza eneo la Mazoezi ambalo litawaleta karibu wakazi wa Bunju, Mbweni, Boko, Tegeta na sehemu za karibu kushiriki michezo mbalimbali lakini kutokana na muitikio mzuri wa diwani wanatumaini kilio hicho kitapata ufumbuzi wa haraka zaidi.

…Mwisho…

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!