Na Shomari Binda-Musoma
DIWANI wa Kata ya Mwigobero manispaa ya Musoma Mariam Sospeter ameridhishwa na ukarabati wa majengo unaofanywa kwenye shule ya msingi Mwembeni iliyo chini ya Kata hiyo.
Akizungumza mara baada ya ziara ya Kamati ya Siasa ya Kata ya Mwigobero ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) iliyofanyika leo januari 21 ameona kazi nzuri inayofanyika.
Amesema kama diwani wa Kata anayepigania miradi ya Kata kwenye vikao vya halmashauri na kuona kazi zinakwenda
Mariam ambaye ni diwani pekee wa Kata Mwanamke kwenye baraza la madiwani amesema Mwigobero ipo salama na viongozi wa chama na serikali wanafanya kazi kwa ushirikiano.
Amesema elimu ni suala la msingi kwenye suala la maendeleo hivyo kuwa na sehemu nzuri ya watoto kusomea ni jambo jema.
Mariam amesema kama kiongozi kupitia ziara hiyo ya Kamati ya Siasa ameridhiswa na ukarabati unaoendelea kwenye majengo ya madarasa.
” Leo tumefanya ziara ya Kamati ya Siasa kwenye shule yetu ya Mwembeni na moja ya maeneo tuliyopitia ni ukarabati wa majengo ya madarasa.
” Wajumbe wametembea wameona hali halisi majengo yanapendeza na wametoa maelekezo palipo na changamoto ili kupendeza zaidi”amesema.
Akizungumzi shughuli za maendeleo za Kata diwani Mariam amesema zinakwenda vizuri zikiwemo shughuli za maendeleo.