Home Kitaifa DIWANI KATA YA MSHEWA AMEISHUKURU SERIKALI KUWAJENGA MABWENI MAWILI KATIKA SHULE YA...

DIWANI KATA YA MSHEWA AMEISHUKURU SERIKALI KUWAJENGA MABWENI MAWILI KATIKA SHULE YA SEKONDARY KWIZU

Mheshimiwa Diwani wa kata ya Mshewa Gaitan Mkwizu amesema wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Sekondari Kwizu kata ya Mshewa Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu baada ya Serikali kujenga mabweni mawili ya wasichana na wavuna wanaotoka maeneo ya mbali.

Awali wanafunzi wengi kutoka kwenye Vijiji vya mbali walikuwa wakipata adha kubwa ya kutembea umbali mrefu. Kwenda shuleni muda mwingine wanachelewa Masomo.

Miongoni mwa Vijiji hivyo vilivyopo mbali na shule hiyo ya Kwizu ni Kijiji cha Goma na Manka kitu ambacho kilipelekea kupoteza ndoto nyingi za watoto wa kike kwani wengi walikuwa wakipata mimba za utotoni Amesema Diwan Gaitan

Aidha nitakuwa mchoyo wa fadhira kama nisipo mshurukur Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa Kazi kubwa anayoifanya Katika kuleta Maendeleo kwenye Taifa letu pia amekuwa na Mchango mkubwa Sana kwa wanafunzi kwa kujenga shule nyingi na mabweni lengo wanafunzi waweze kutimiza Ndoto zao walizonazo hasa kwa watoto wa kike.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!