Diwani wa viti maalum Halmashauri ya Kibaha vijijini Mheshimiwa Josephine Gunda amekabidhi kilo 800 za unga kwa Wanafunzi wa Shule za msingi na sekondari za Kata ikiwa ni uzinduzi wa kampemi yake ya NISHIBISHE akilenga uahamasishaji wa wazazi na wadau mbalimbali kusaidia kuchangia vyakula mashuleni ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi Shuleni.
Ambapo katika uzinduzi huo Mheshimiwa Josephine amekabidhi kilo 800 hizo katika shule ya sekondary Gwata wakati wa uzinduzi huo.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo ndugu David Mramba ambaye ni Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Pwani amesisitiza wazazi kuendelea kuchangia chakula kwaajili ya watoto ili wanafunzi waepukane na vishawishi vinavyoweza kusababisha ukatili wa kijinsia pamoja na mimba mashuleni kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Diwani wa viti maalum Ndg. Josephine Gunda ameeleza lengo la Kampeni hiyo huku mwenyekiti Wa Halmashauri ya Kibaha Vijijini akiwataka wazazi kuwa mstari wa mbele kuchangia vyakula mashuleni.
Josephine amesema unga huo ni kwaajili ya kuugawa kwenye kata mbili za Magindu na Gwata zenye jumla ya shule 7 za msingi na shule mbili za Sekondari wamenufaika na huo unga.
“Unga huu ni kwa shule 9 Shule 7 za msingi na shule 2 za secondary”
“Lengo la kampeni hii ni kuongeza kiwango cha ufaulu na kupunguza utoro mashuleni kwasababu mtoto hawezi kusoma akiwa na njaa” amesema Josephine.
“Pia kampeni hii ni njia moja wapo yakuhamasisha wazazi na wao walipe kipaumbele suala la kuchangia chakula mashuleni” amesema.
Tukio hilo limeongozwa na Mgeni rasmi mheshimiwa David Mramba Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Pwani akiambatana na Mwenezi wilaya ya Pwani na wadau wa Smaujata pamoja na See foundation.
Mheshimiwa Mramba pamoja na kuzindua kampeni hiyo pia ameshiriki kupanda mti na zoezi hilo limefanywa na Viongozi mbalimbali akiwemo Josephine na Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya ikiwa ni miti ya kumbukumbu ya tukio hilo.
Mheshimiwa Mramba akihutubia mkutano huo aliwataka Wazazi kusema mambo yanayofanywa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini.