Home Kitaifa DIWANI GOLDEN AWAHUSIA WAHITIMU MOREMBE SEKONDARI KUJIEPUSHA NA USHOGA NA MAPENZI YA...

DIWANI GOLDEN AWAHUSIA WAHITIMU MOREMBE SEKONDARI KUJIEPUSHA NA USHOGA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Na Shomari Binda-Musoma

WANAFUNZI wahitimu wa kidato cha 4 wa shule ya sekondari Morembe wametakiwa kutojihusisha na vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja.

Kauli hiyo imetolewa na diwani wa Kata ya Kitaji na mlezi wa shule hiyo, Golden Marcus wakati wa mahafali ya 25 ya shule hiyo.

Amesema katika kipindi cha siku za hivi karibuni kumeibuka vitendo ambavyo ni vya aibu ikiwa ni vijana wa kiume kujihusisha na ushoga na usagaji kwa watoto wa kike.

Golden amesema kitakuwa kitrndo cha aibu kusikia mwanafunzi kutoka Mormbe anashiriki kwenye vitendo hivyo.

Amesema kama mlezi wa shule hiyo hategemei kusikia na kupata taarifa za vitendo vilivyo kinyume na maadili.

Akizungumzia masuala ya kitaaluma diwani huyo amewapongeza walimu kwa kusimamia vizuri na kupata matokeo mazuri kwenye mitihani.

Amesema kwa mujibu wa taarifa ya shule upo uhakika wa kufanya vizuri na kuendelea na masomo ya elimu ya juu.

Aidha katika kujibu risala ya shule hiyo amesema changamoto zilizoelezwa zitakwenda kufanyiwa kazi moja baada ya nyingine na hivi karibuni jumla ya madarasa 10 yatajengwa kwenye shule hiyo.

Mkuu wa shule hiyo Rafael Katikiro ameishukuru serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia milioni 8 kwa ujenzi wa madarasa mapya 4 ambayo wameanza kuyatumia.

Amesema katika kipindi cha miaka 5 iliyopita shule imefanya vizuri na kuamini katika mitihani ya mwaka huu watafanya vizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!