Na Mwandishi Wetu
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na mafunzo ya Ufundi Stadi ( NACTVET ) limetoa Ithibati kwa Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam ( DIT ) , KUDAHILI , KUFUNDISHA , KUTAHINI na KUTOA TUZO kwa Shahada ya Kwanza ya Uhandisi wa Vifaa Tiba ( Bachelor Of Engineering in Biomedical Equipment )
Akizungumza mapema leo hii Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma DIT Bwn. Amani Kakana amesema amesema Shahada hii ni ya miaka mitatu na itaanza kutolewa katika mwaka ujao wa masomo yaani 2023 / 2024 ambao unatarajiwa kuanza katikati ya mwezi Oktoba , 2023 na walegwa ni Wahitimu wenye sifa zifuatazo
1. AWE NA CHETI CHA UFUNDI SANIFU KATIKA UHANDISI WA VIFAA TIBA
2. WAHITIMU WA STASHAHADA YA UHANDISI WA VIFAA TIBA
3. WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA WENYE UFAULU WA HESABU , FIZIKIA NA KEMIA KWA WASTANI WA ALAMA 2.5
” Serikali ya awamu ya sita imefanya maboresho makubwa katika sekta ya Afya kwa kujenga miundo mbinu na kusambaza vifaa Tiba vya kisasa katika hospitali na vituo vya afya kote nchini , kwahiyo wahitimu wa Shahada hii ndio wanaotegemewa kuvikarabati vifaa ivyo ili vikae katika hali ya ubora , lakini pia wahitimu baada ya mafunzo watakua na ujuzi wa kutengeneza viungo bandia vitakavyowasaidia wenzetu watakaopata changamoto ya kupoteza viungo vyao kwa sababu mbalimbali “ Amesema Bwn. Kakana
Dirisha la Usajili lipo wapi unaweza kujisajili kupitia https://admission.dit.ac.tz/admission/apply
na dirisha litafungwa Oktoba 6, 2023.