Home Kitaifa DIBIBI AGAWA VIFAA VYA OFISI KWA MAKATIBU KATA NA MATAWI YA JUMUIYA...

DIBIBI AGAWA VIFAA VYA OFISI KWA MAKATIBU KATA NA MATAWI YA JUMUIYA YA WAZAZI KISARAWE

Na Scolastica Msewa, Kisarawe

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kisarawe Khamisi Dibibi akabidhi vifaa vya ofisi za Jumuiya kwa Makatibu kata na matawi vyenye thamani ya zaidi ya shillingi milioni 9 ikiwa ni mkakati wa kukijenga Chama cha Mapinduzi wilayani humo.

Amesema hayo kwenye mkutano wa Jumuiya hiyo ngazi ya wilaya ambapo Kaimu Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Pwani Sophia Abdul alikuwa Mgeni rasmi.

Dibibi vifaa alivyokabidhi ni reflector kwa Viongozi wote wa kata za wilaya ya Kisarawe, Kadi za jumuiya ya wazazi 300 kila tawi kwa matawi 119, stap pad (Kidawu) kwa matawi yote 119 na kata 17.

Amesema pia amekabidhi leja za kusajilia wanachama kwa matawi yote 119, mihuri ya matawi yote 119 na kata zote 17.

Dibibi katika mkutano huo amewataka Makatibu kata na matawi kuanza maandazi ya chaguzi za serikali za mitaa kwa kuhimiza wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea Uongozi muda utakapofika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!