Home Kitaifa Dereva aliyesababisha vifo sita kikundi cha Aden Palace akamatwa

Dereva aliyesababisha vifo sita kikundi cha Aden Palace akamatwa

Jeshi la police mkoani mwanza linamshikilia Oswald kaijage binamungu miaka 39, mhandisi wa umeme katika mgodi wa Geita Gold Mining (GGM)aliyetoroka baada ya kusababisha ajali siku ya Jumamosi julai 22,2023 eneo la Lumala Barabara ya Kiseke Wilaya ya ilemela Mkoani Mwanza

Akizungumza na Waandishi wa habari kamanda wa police Mkoani Mwanza wilbord Mutafungwa amesema mtuhumiwa aliwagonga kuwa ajali hiyo ilihusisha gari yenye namba ya usajili T.476 aina ya Toyota Hilux Double Cabin Kwa kuwagonga watu waliokuwa wanafanya mazoezi ya Mchakamchaka kikundi cha kukimbia cha Aden (joggingClub) katika barabara iyo

Hata hivyo jeshi la police mkoani mwanza limeshauri vikundi vya mchakamchaka kusajili vikundi vyao katika ofisi za wilaya/au Jiji ambapo watapewa miongozo au maelekezo ya manma ya kufanya mazoezi Kwa kuzingatia hali ya usalama wao na watu wengine

Jeshi la police mkoani mwanza linakumbusha vikundi hivyo kutoa taarifa Kwa jeshi la police endapo wataitaji kutumia Barabara wakati wa mazoezi yao ili askari wa usalama barabarani waweze kusimamia usalama wao na watumiaji wengine wa barabara ambayo Kwa wakati huo watakuwa wanatumia barabara hizo ili kuepusha ajali.

Pamoja na hayo jeshi Hilo mkoani mwanza limeita viongozi wote wa jogging clabu siku ya Jumamosi julai 29 mwaka huu majira ya saa moja asubuh katika uwanja wa michezo nyamagana ili kufika Kwa ajili ya kupata elimu zaidi ya usalama barabarani na mambo muhimu ya kuzingatia wakiwa barabarani wakati wa kukimbiza ili kuepusha ajali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!