Home Biashara DED TEMEKE AWAASA WANACHI KUPUUZA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI JUU YA UTOAJI WA...

DED TEMEKE AWAASA WANACHI KUPUUZA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI JUU YA UTOAJI WA MIKOPO YA 10%

Na Magrethy Katengu

Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke ndugu Elihuruma Mabelya amewataka Wananchi kupuuza taarifa za Upotoshaji zinazosambazwa kuhusu utoaji wa mikopo 10% kwa vijana,wanawake,na watu wenye ulemavu.

Ameyasema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa na mmoja wa waandishi wa habari alipotembelea banda la Manispaa hiyo Agosti mwaka huu katika maonesho ya Wakulima(Nanenane) mkoani Morogoro,Mkurugenzi Mabelya amesema kuwa taratibu zote za utoaji wa mikopo hiyo hufuatwa kama alivyoagiza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

“Niwakikishie kuwa utoaji wa mikopo upo vizuri ,hakuna kikundi chochote kinachopendelewa, utaratibu unaanzia kwenye kata husika , kikundi kinatakiwa kiandae andiko au dokezo hivyo ukweli ni kwamba utoaji wa mikopo hii hufuata sheria na kanuni”.mesisitiza Mabelya.

Awali akikagua baadhi ya shughuli zinazofanywa katika banda la Manispaa ya Temeke,mkurugenzi Mabelya alionesha kufurahishwa kwake mara baada ya kupata maelezo ya kina kutoka kwa wataalamu wa kilimo,mifugo na Uvuvi namna wanavyotoa huduma kwa wananchi.

Moja ya matunda ya mikopo inayotokana na 10% ya mapato ya ndani ya Manispaa ni Wajasiriamali ambao wameshiriki katika maonesho ya Nanenane mkoani hapa, ambapo wameweza kuleta bidhaa zao kuzitangaza na kuuza ili kujiongezea mapato.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!