Home Kitaifa DED MOSHI AAGIZWA KUMCHUKULIA HATUA MHANDISI WA UJENZI KWA KUKWAMISHA MIRADI

DED MOSHI AAGIZWA KUMCHUKULIA HATUA MHANDISI WA UJENZI KWA KUKWAMISHA MIRADI

Na: OR-TAMISEMI, Moshi

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Shadrack Mhagama kumchukulia hatua za kinidhamu Mhandisi Ujenzi wa Halmashauri hiyo Daniel Kileo kwa kushindwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa ya mradi wa BOOST kinyume na maelekezo ya Serikali yaliyotolewa na TAMISEMI.

Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo, mara baada ya kutoridhishwa na ujenzi wa madarasa akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi inayojengwa na Serikali kupitia mradi wa BOOST na SEQUIP.

Mhe. Ndejembi amesema, haiwezekani Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atafute fedha za kujenga miundombinu ya elimu alafu zisitumike vizuri kwa sababu ya Mhandisi wa Wilaya kushindwa kutafsiri ramani wakati yeye ndiye mtalaam na mwenye jukumu hilo.

“Mkurugenzi mchukulie hatua za kinidhamu Mhandisi wa Ujenzi na mkaimishe mwingine kwani huyu ameshindwa kusimamia ujenzi wa madarasa na Ofisi ya Rais TAMISEMI itakuletea Mhandisi mwingine atakayesimamia miradi ya ujenzi ya miundombinu ya elimu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Baada ya ukaguzi wa Miradi ya Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Mhe. Ndejembi amebaini kuwa miradi mingi katika Halmashauri hiyo haijakamilika wakati katika Wilaya nyingine ikiwemo Manispaa ya Moshi imeshakamilika na changamoto kubwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ikiwa ni kuwa na Mhandisi ambaye ameonekana kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Aidha, Mhe. Ndejembi amesema amepewa taarifa kuwa katika shule ya Sekondari Ashira bweni moja halijajengwa licha ya kuwa fedha zilitolewa na Serikali na Mhandishi huyo kushindwa kusimamia ujenzi huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!