Home Kitaifa DCEA yateketeza kilo 1543 za madawa ya kulevya.

DCEA yateketeza kilo 1543 za madawa ya kulevya.

Na Hadia Khamis,
Mamlaka ya kupambana na kuzuia Dawa za Kulevya nchini DCEA imeteketeza Dawa mbalimbali za kulevya takribani Kilogram 1543 katika kiwanda Cha Saruji kilichopo wazo jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Kamishna Jeneral wa DCEA, kamishina wa kitengo cha huduma za sheria Veronica Matikila amesema uteketezaji huo hufanyika mara baada ya mashauri ya dawa za kulevya kuwa yamekamilika mahakamani.

Hii ni mara ya pili kufanya zoezi hili,Mara ya kwanza tulifanikiwa kutekeleza dawa hizi za kulevya katika kiwanda Cha dangote na tunateketeza katika viwanda hizi kwa lengo la kutoharibu Mazingira lakini pia kwa kuweka usalama na ndio maana hapa mnawaona viongozi mbali mbali pamoja na jaji,“amesema Matikila.

Pia ametaja mchanganuo wa Dawa za kulevya zilizotekezwa ambazo ni heloini na kokeini jumla ya Kilogram 569, tani mbili za bangi.

Aidha amesema Dawa za Kulevya zilizotekezwa zimetoka katikati mahakama mbalimbali ikiwemo mahakama kuu kanda ya Dar es salaam,mahakama kuu Division ya uhujumu uchumi pamoja na rushwa,mahakama ya hakimu mkazi kisutu,mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa pwani pamoja na mahakama za wilaya.

Hata hivyo ameitaka Jamii kuendeleza kutoa ushirikiano wa kuhakikisha watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya wanakamatwa kwa kuwa Tanzania bila ya dawa za kulevya inawezekana.

Amesema Tanzania ni nchi salama na yenye utulivu hivyo watahakikisha wafatilia minendo ya wauzaji dawa za kulevya bila kusita usiku na mchana ili kuhakikisha taifa linabaki salama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!