ANNA RUHASHA Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga amewatahadhalisha wazazi na walezi watakaokaidi kuwapeleka watoto waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza 2023 watachukuliwa hatua kali za sheria ikiwa nipamoja na kufikishwa mahakamani.
Senyi ametoa kauli hiyo mapema katika hafla fupi ya kupokea vyumba vya madarasa 152 vilivyojengwa kwa Bilioni3,040,000,000.00 katika shule za sekondari 31.
Aidha,ameongeza kwa kusema kuwa haiwezekani serikali inajenga vyumba vizuri vya madarasa na kutoa elimu bure alfu wazazi wanashindwa kuwapeleka shule kwa kisingizio tu mtoto amegoma kwa mwaka huu amesema watamuelewa.
Awali kaimu mkurungenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema ,Mwita Waryuba katika taarifa ya kukabidhi vyumba 152 kwa mkuu wa wilaya amesema kuwa ujenzi wa vyumba hivyo umekamilika kwa asilimia 95 huku vyumba nane vikiendelea kukamilishwa ndani ya muda uliyotolewa vitakuwa navyo vimekamilika .
Pia ameongeza wingi wa vyumba vya madarasa katika halmashauri hiyo kwa kiwango kikubwa vitapunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Akizungumza kwa niaba ya madiwani pamoja na wananchi mwenyekiti wa halmashauri Yanga Makaga ametumia nafsi hiyo kumshukuru Mh Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia huku akitumia nafasi hiyo kutazama pia shule za msingi.
Hata hivyo kwa jumla ya wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2023 katika halmashauri ya Sengerema 9,703
Mwisho