Home Kitaifa DC SIMA ALIPONGEZA NA KULISHUKURU SHIRIKA LA TEKLA, LATOA MSAADA KWA WATOTO...

DC SIMA ALIPONGEZA NA KULISHUKURU SHIRIKA LA TEKLA, LATOA MSAADA KWA WATOTO 50 WENYE ULEMAVU BUKOBA

Na Theophilida Felician Kagera.

Mkuu wa wilaya Bukoba Erasto Sima amelipongeza shirika linalojihusisha na masuala ya watu wenye ulemavu nchini TEKLA kwa namna lilivyowiwa na kuamua kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya mahitaji ya shule kwa wanafunzi wenye ulemavu wa baadhi ya shule za msingi katika Halmashauri mbili za wilaya ya Bukoba mkoa Kagera.

Akitoa pongezi na shukrani hizo akiwa Mgeni rasmi katika shughuli ya kukabidhi vifaa hivyo kwa walengwa iliyofanyika Shule ya msingi Tumaini kata ya Kashai Manispaa ya Bukoba amesema kuwa jambo lililofanywa na shirika hilo la kuwakumbuka watoto hao ni jema mno katika jamii.

Ndugu zetu wa Tekla mimi ni washukuru kwa jambo hili mumelilona mulifanye ni jambo la kiimani ni jambo la kihuduma ni jambo ambalo ni sadaka, ni washukuru sana sana” amesisitiza Mkuu wa wilaya Sima.

Pia amesema kuwa Serikali katika utekelezaji wake wa ujenzi wa miradi ya maendeleo imekuwa ikiyakumbuka kwa namna mbalimbali makundi yenye mahitaji maalumu likiwemo kundi la watu wenye ulemavu hususani ujenzi wa miundombinu mahususi ikiwemo ya vyoo shuleni ili kuwasaidia wanafunzi wa namna hiyo kuepuka changamoto wanazokumbana nazo wakati wanapokuwa wanahitaji huduma ya kujisitiri.

Hata hivyo ameahidi kuendelea kushirikiana na makundi yote ya watu wenye ulemavu katika mambo mengi zikiwemo siku za matukio ya kusherehekea sikukuu za makundi hayo huku akiwapongeza wazazi na walezi kwa jinsi wanavyoendelea kuwalea vyema watoto wao bila ya kuwatenga hatimaye watoto hao wanaendelea kusoma vizuri shule tofauti tofauti katika wilaya hiyo ya Bukoba.

Mtendaji Mkuu wa shirika hilo Mugisha Kasaju amesema kuwa Tekla wametoa vifaa hivyo kwa wanafunzi hao 50 kwa malengo ya kuwasaidia kupunguza changamoto walizonazo za uhaba wa mahitaji muhimu ya kuwawezesha kusoma vyema shuleni.

Amevitaja baadhi ya vifaa walivyovitoa ni pamoja na Baiskeli za magurudumu matatu( 3) viti mwendo, sale za shule na vifaa maalumu kwa ajili ya kufundishia watoto, vitu ambavyo vimeghalimiwa jumla ya zaidi ya Sh Milioni 17.

Amehitimisha akisema licha yakuwafikia hao bado wapo walengwa wengine wenye changamoto zaidi zinazohitaji mpango zaidi hivyo juhudi zinahitajika kuweza kuwafikia ili kutatua changamoto zao ambapo ameahidi na kusema kwamba wao kama Tekla wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuwasaidia wananchi hasa watu wenye ulemavu.

Mmoja wa wazazi waliokuwa wameambata na watoto wao mama yake na mtoto Meli Daud ambaye amepata kiti mwendo wamelishukuru shirika la Tekla kwakuwasaidia watoto wao vifaa hivyo muhimu kwani ni changamoto nyingi wanazozipitia watoto wao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya uwezo mdogo wa kifedha kwa wazazi na walezi hali inayopelekea watoto wengi kukosa huduma muhimu ikiwemo ya elimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!