Home Kitaifa DC. SHAKA: TUNAKUJA NA MPANGO MAALUM WA KUWAELIMISHA WANANCHI

DC. SHAKA: TUNAKUJA NA MPANGO MAALUM WA KUWAELIMISHA WANANCHI

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka akiongea na waandishi wa habari juu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya RUDEWA-KILOSA kwa kiwango cha lami

Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, iko mbioni kuja mpango maalum kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi bora na utunzaji wa barabara ya RUDEWA-KILOSA ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kila mwananchi aweze kufaidika nayo .

Hayo yamesemwa Aprili 16, 2023 na Mkuu wa Wilaya hiyo, Shaka Hamdu Shaka akiongea na waandishi wa habari na kueleza kuwa ujenzi wa barabara hiyo umekamilika kwa asilimia 90.

Shaka ameongeza kuwa, kukamilika kwa barabara hiyo kutaimarisha hali ya uchumi wa Kilosa na uchumi wa wananchi na mwananchi mmoja mmoja.

Kukamilika kwa barabara ya RUDEWA-KILOSA itakwenda kuimarisha hali ya uchumi wa Kilosa na uchumi wa wananchi na mwananchi mmoja mmoja na Kilosa itakwenda kubadilika kufuatia ujio wa miradi mikubwa kama hii ya ujenzi wa miundombinu ya barabara” alisema Shaka na kuongeza

Namshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha nyingi karibu shilingi bilioni 32.9 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Rudewa hadi Kilosa”

Ujenzi wa barabara ya Rudewa unatekelezwa na mkandarasi Umoja Kilosa JV unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, mwaka huu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!