Ashrack Miraji Kilimanjaro
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewataka wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 kujiepusha na vitendo vya Rushwa wakati wanapotekeleza majukumu yao kwenye kipindi chote cha zoezi la Uchaguzi kwani Rushwa ni adui wa haki na hudumaza maendeleo kwenye jamii.
DC Kasilda amezungumza hayo wakati akifungua Semina ya mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 unaotarajiwa kufanyika Novembea 27, ambapo amesisitiza uzingatiaji wa miongozo na kanuni za Uchaguzi zilizotolewa na Wizara ya TAMISEMI kwenye Halmashauri.
“Hii ni kazi maalum ambayo mnaenda kuitenda, mnaenda kuwaongoza Wananchi niwaombe sana watumishi wenzangu kaepukeni masuala ya Rushwa, Rushwa ni adui wa haki na hudumaza maendeleo kwenye maeneo yetu. kanuni za utendaji wa utumishi wa uma zinakataa mtumishi kujihusisha na masuala ya Rushwa na mambo mengine ambayo yatakushushia hadhi kama mtumishi wa uma”. Alisema DC Kasilda.
Aidha ameelekeza Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha kuwa wanaenda kuhamasisha kikamilifu Wananchi waijue vizuri ratiba na matukio yote ya Uchaguzi kwa njia zozote zile ambazo wanazitumia kufikisha jumbe na taarifa mbalimbali za Serikali kwenye maeneo yao kwa kuzingatia maslahi makubwa ya Nchi