Home Kitaifa DC SAME AMEWATAKA WANANCHI NA WAUMINI WA DINI KIKRISTO KUSHEHEKEA PASAKA KWA...

DC SAME AMEWATAKA WANANCHI NA WAUMINI WA DINI KIKRISTO KUSHEHEKEA PASAKA KWA AMANI NA UTULIVU

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amewataka Wananchi na Waumini wa dini ya Kikristo kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa kuendelea kudumisha amani, upendo na mshikamano.

Mkuu huyo wa Wilaya ameyasema hayo Jana wakati akizungumza na Waumini wa dini ya Kikristo kwenye ibada ya Pasaka Kanisa la T.A.G BATHEL REVIVAL TEMPLE.

Aidha amewataka Waumini hao kutumia fursa hii ya ibada Pasaka kuendelea kuiombea nchi ambayo itaingia kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivi karibuni, lakini pia kuendelea kumwombea Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mungu amlinde dhidi ya maadui wa nchi yetu na andelee kuliongoza vyema Taifa.

Lakini pia amewaomba Viongozi wa dini baada ya kumaliza kuongoza ibada kuwatangazia Waumini wote kujitokeza kwa Wingi kushiriki kuupokea Mwenge wa Uhuru ambao Kitaifa unatarajiwa kuzinduliwa April mbili kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro na sisi Wilaya ya Same tutaupokea April nane pale shule ya Msingi Njoro ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga.

Shime shime Wananchi tujitokeze kwa wingi siku hiyo kuushangilia Mwenge wetu wa Uhuru, lakini pia niwakaribishe kwenye Mkesha wa Mwenge pale Shule ya Msingi Hedaru kutakuwa na mada mbalimbali kutoka kwa wataalam waliondaliwa bila kusahau burudani kutoka kwa wasanii nguri wa muziki wa Kizazi kipya“.

Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu umebeba kauli mbiu isemayo “Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu“.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!