Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangasa leo tarehe 05 Oktoba, 2022 ameungana na Baraza la Wazee la Wilaya ya Kigamboni katika kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani Wilayani Kigamboni ambapo kitaifa ilifanyika tarehe 01 Oktoba Jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Mjimwema ambapo yalibeba Kauli Mbiu isemayo ” Ustahimilivu na Mchango wa Wazee ni muhimu kwa Maendeleo ya Taifa “
Katika Viwanja hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameendesha Zoezi la utoaji Elimu Lishe na Matibabu bure kwa wazee wetu.
DC Nyangasa ameielekeza Manispaa ya Kigamboni kusimamia vema mabaraza ya wazee na kuhakikisha Inatenga kiasi cha fedha kila Mwaka kutoka mapato yake ya ndani kwaajili ya kulipia Bima za wazee wasio na uwezo katika jitihada za kusaidia kundi hilo Muhimu kupata matibabu kwa wakati.
“Mhe. Rais wetu Samia Suluhu Hassan anawatambua wazee wetu na amekuwa akitoa maelekezo na uwezeshaji katika hatua mbalimbali kuhakikisha changamoto zinazowakabili wazee wetu zinapatiwa ufumbuzi hatua kwa hatua. Anawapenda na kuwathamini sana wazee wetu”
Kigamboni ina takriban wazee 5000 wanaotambulika kwenye mfumo rasmi , huku matokeo ya Sensa ya watu na makazi iliyofanyika Mwaka huu yakitarajiwa kutoa idadi halisi ya kundi hili katika wilaya ya Kigamboni.